TIGO NA HAJI MANARA KUMWAGA ZAWADI ZA PESA , SIMU NA MAGARI KWA WATEJA WAO .... SOMA HAPA
Na Adery Masta.
Dar es Salaam, Novemba 7, 2024 – Katika kuelekea msimu wa sikukuu, Tigo, kampuni inayoongoza kwa huduma za maisha ya kidijitali nchini Tanzania, imezindua kampeni mpya ya “Magifti ya Kugifti” yenye lengo la kusherehekea miaka 30 ya kuungana na wateja, mawakala, na wafanyabiashara wake. Kampeni hii ya wiki 13 au siku 90 ni sehemu ya utamaduni wa Tigo kutoa shukrani kwa wateja wake kwa kuwazawadia zawadi za kipekee ambazo zitaleta furaha kwao na wapendwa wao msimu huu wa sikukuu.
"Magifti ya Kugifti" inaakisi shukrani za dhati za Tigo kwa wateja wake milioni 23.5 ambao wamechangia pakubwa katika ukuaji na mafanikio ya kampuni hii. Kupitia kampeni hii, Tigo inalenga sio tu kutoa zawadi za thamani bali pia kukuza mahusiano ya kijamii na kutengeneza kumbukumbu nzuri.Katika kipindi chote cha kampeni ya Magifti ya Kugifti, wateja wa Tigo wana nafasi nyingi za kushinda zawadi za kuvutia. Kila siku, wateja wanaweza kujishindia hadi TSh milioni 1 pamoja na simu janja sita kila siku—jumla ya simu 540 zitakazotolewa katika kampeni hii. Pia, kuna droo za kila wiki zenye zawadi ya TSh milioni 5, wakati droo za kila mwezi zitatoa TSh milioni 10 na gari mpya aina ya KIA Seltos kwa mshindi mmoja atakayebahatika. Wateja wanaonunua vifurushi vya sauti watajipatia bonasi za papo hapo, na miamala ya Tigo Pesa itawawezesha kupata pointi ambazo wanaweza kuzibadilisha kwa dakika, SMS, na data. Mawakala na wafanyabiashara wa Tigo Pesa pia wanayo nafasi ya kushinda TSh milioni 1 kila wiki.
Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, alisisitiza umuhimu wa kuthamini wateja kwa kusema, “Kwetu sisi kutoka Tigo Pesa, wateja wetu ndio msingi wa kila kitu tunachofanya. Magifti ya Kugifti ni shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja wao. Tunapofunga mwaka, tunataka wateja wetu wajione wanathaminiwa na kuwezeshwa, wakifahamu kuwa uaminifu wao unachangia ndoto yetu ya yakuiona Tanzania inasonga mbele katika swala zima la matumizi ya huduma ya matumizi ya fesha kupitia simu za mkononi. Ni heshima kubwa kuweza kurudisha kwa zawadi zinazowasaidia kutimiza ndoto zao wao na wapendwa wao.”Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Isack Nchunda, alionesha furaha yake kuhusu msimu huu wa kutoa na kutafakari safari ya Tigo kwa miaka 30 iliyopita. “Mwaka huu umekuwa wa kipekee,kwa kunipitia ubunifu, niseme tu shukrani kwa imani ambayo wateja wetu wanayo kwetu. Uwekezaji wetu unaoendelea wa 4G na 5G kote nchini Tanzania unatuwezesha kutoa suluhisho zinazorahisisha maisha ya kila siku. Kupitia Magifti ya Kugifti, tunasherehekea miaka 30 ya kuungana na wateja wetu na kuwashukuru kwa zawadi zinazowaleta karibu na kuinua jamii nzima.”
Kushiriki kampeni hii ni rahis,; wateja wanachotakiwa kufanya ni kufanya miamala ya Tigo Pesa au kununua vifurushi vya sauti kupitia njia yoyote ili kujiunga na kujishindia zawadi hizi kem kem Mawakala na wafanyabiashara(Lipa Kwa Simu) wanaweza kushiriki kwa kufikia viwango maalum vya miamala, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Tigo kusaidia ukuaji wa wadau wake.
“Magifti ya Kugifti” inaonesha dhamira ya kampuni ya kuongeza tafrija za mwisho wa mwaka na kuwezesha wateja, mawakala, na wafanyabiashara kumaliza mwaka kwa furaha na kuanza 2025 kwa matumaini na ari mpya.
No comments