Breaking News

MAGIFTI YA KUGIFTI , 84 WASHINDA SIMU JANJA NA ZAIDI YA 30 WASHINDA MAMILIONI

PICHA YA PAMOJA : Novemba 22 , 2024 : Baadhi ya Washindi wa simu janja na Pesa Taslimu Hadi Milioni 5 ( Wateja na Mawakala wa Tigo ) katika KAMPENI ya Magifti ya Kugifti , wakiwa katika picha ya Pamoja na Semaji la Kampeni hii Haji Manara . Ikumbukwe Hadi Wiki hii ya pili Tigo wametoa zawadi za Simu kwa Wateja wao 84 , na Washindi wa Pesa Taslimu Milioni Moja Hadi Milioni Tano kwa Washindi ambao ni Wateja 16 , na Washindi wafanya biashara 15 , ili kuibuka mshindi unachotakiwa ni kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania, imeendelea kuonyesha upendo kwa Wateja Wake na Wafanyabiashara wanaopokea Malipo kwa  Lipa Namba ya Tigo, kupitia Kampeni yake ya Magifti ya Kugifti Kampeni ya Mwisho wa Mwaka iliyozinduliwa Wiki mbili zilizopita na Kampuni ya Tigo itakua ikitoa zawadi za  Simu Janja na Fedha Taslimu Milioni 1 - 5 , kwa Wateja na Wafanyabiashara nchi nzima kwa Wiki 13 za Kampeni hii. 

Akizungumza wakati wa Kutoa zawadi kwa Baadhi ya Washindi kutoka Dar Es Salaam waliofanikiwa kufika makao Makuu ya Tigo kukabidhiwa zawadi zao Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Bwn. Eginga Mohamed amesema 

                         

" Kampeni hii itadumu ndani ya Wiki 13 na ndo kwanza tupo wiki ya Pili kwahiyo watumiaji wa Mtandao wa Tigo kote Nchini bado wana nafasi ya kushinda Pesa Taslimu Milioni 1- 5 na Simu janja Kila siku , unachotakiwa kufanya ni miamala ya Tigo ya Pesa , Nunua Muda wa Maongezi , LUKU , Lipa kwa Simu n.k ili ujizolee pointi za Kushinda Pesa Hadi Milioni 5 na Simu Janja Kila siku " amesema Eginga. 

                         

Ramadhan Iddi Ikupa Mkazi wa Kinondoni Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa Washindi  wa Milioni Moja Wiki hii ya Pili , akizungumza na Mwandishi Wetu kwa furaha kubwa ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kuwazawadia Fedha hiyo , maana kwa Upande wake itamsaidia kumnunulia mwanae Mahitaji mbalimbali ya Shule maana anatarajia kuanza kidato cha Kwanza Januari.

                           

                            

.

No comments