Breaking News

TIGO WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Mawasiliano, TIGO Tanzania katika kuelekea kufunga mwaka, wametoa msaada wa vitu mbalimbali  kwenye kituo cha Sinza maalumu kilichopo jijini dar es salaam chenye watoto zaidi ya 93.

Akizungumiza mara baada ya kutoka msaada huo Mkurugenzi wa Tigo  Dar es salaam,  Bw. Aidan Komba amesema kama TIGO Tanzania wanatambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalumu na kuona kunaulazima wa kurejesha Kwa jamii faida wanayoipata.

Msaada iliyotolewa kituoni hapo ni pamoja na charahani, magodoro, chupa, mahotipoti kwaajili ya kuhudumia jamii hiyo yenye uhitaji maalumu.

Sanjali na hayo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Catherine Msese ametoa shukrani zake Kwa kampuni ya TIGO Tanzania Kwa msaada  waliowapatia kwaajili ya shule hiyo

" Kwa kweli msaada huu utawasaudia watoto kujimudu katika kufanya kazi zao za Kila siku kwani tumepata vifaa vya usafi, vitawasaidia watoto katika kufanya usafi hapa shuleni na vifaa vya cherehani vitawasaidia katika mafunzo ya ufundi" alisema


Kampuni ya TIGO Tanzania katika kuendeleza kurudisha Kwa jamii , itaendelea kutoka huduma hizo Kwa Kanda zote tisa nchini ambapo Leo wameanza kwenye Kanda hii ya Dar es salaam.

Aidha msese ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kuishi kwa kupendana ikiwemo kuwa karibu na watoto na jamii yenye nahitaji maalum ili kurudisha shukran kwani kwa kufanya hivyo Kuna mpendeza Mungu


Tigo Tanzania imekuwa mstari mbele katika Kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihimiza watanzania kupendana na kushirikiana kwani Tanzania ni nchi yetu sote 

Kwa sababu hiyo, timu yetu ya Kanda ya Dar Kaskazini, kwa moyo mkunjufu, imejitolea kuleta misaada ya mahitaji muhimu hapa Sinza Maalum, ikiwa ni pamoja na magodoro, mito, mashuka, vifaa vya kusafisha, na hata mashine za kushonea kwa wale wanaotaka kujijengea uwezo wa kujiajiri. Hii sio tu msaada, bali ni ishara ya upendo, mshikamano, na matumaini kwa watoto na ndugu zetu hapa kituoni











No comments