Breaking News

Magift ya Kugift ya Mix by Yas yapamba Moto

 


Na Mwandishi wetu

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS, ikishirikiana  na kitengo cha Mixx by Yas ,Leo hii Novemba 30,2024, imekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi 7 wa Shindano la “Magift ya kugift” kwa wiki ya 3 ambapo kati ya hao 6 wamejishindia  kiasi cha Shilingi Milioni 1 kila mmoja 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Afisa mkuu Mixx by Yas Bi. Angelika Pesha amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi kwa wiki ya tatu 3 nakudai kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.

Pesha amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 35 kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo,mawakala,na wateja wengine.

Kwa upande wake Sia Martin Mlay ambaye amejinyakulia kiasi cha Shilingi mili 5i “amemshukuru Yas kwa  kuchezesha kampeni hiyo ya "MAGIFT ya KUGIFT 2024" na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaisha kila mtu anashinda kutokana na bahati yake amesema Mlay.

Nao baadhi  ya washindi wengine ambao wamejishindia zawadi ya TSh Milion 1  wamemshukuru kwa kupata zawadi zao,  ambapo wengi wao Wamesema, pesa hizo wanakwenda kuziendeleza huku wengine wakiahidi kwenda kulipia ada za shule na huduma nyingine  muhimu.

Kampuni ya YAS imekuwa na muendelezo mzuri WA kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza itakumbukwa kuwa kampuni ya YAS ilizinduliwa hivi karibuni ikichuka pahala la Tigi ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 30 ikitoa huduma zake hapa nchini, na kutunukiwa Tuzo mbali mbali ndani na Nje ya nchi.

Kwa upande wake Balozi wa Yas Tanzania Haji Sunday manara amewataka wateja WA Yas kuendelea kutuma miamala kupitia simu zao ili wawe kwenye nafasi nzuri za kujishindia zawadi nyingi, na amesema Wazi kuwa hakuna longol ongo kwenye kampeni hii ya MAGIFT ya KUGIFT, hivyo kila mtu anaweza kuibuka mshindi siku yake ikifika.

Hii ni wiki ya tatu mfulululizo kati kati ya wiki 12 ambazo Yas kupitia msimu huu wa siku kuu Yas  imepanga kutoa zawadi Zaidi kupitia kampeni Yao ya Magift ya kugift kwa mwaka huu wa 2024.


No comments