SEMINA ZA KIBOKO PAINTS ZAWAFIKIA MAFUNDI KAHAMA
Na Adery Masta.
Kampuni namba moja nchini kwa Utengenezaji , Uuzaji na Usambazaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujenzi kama vile Mabati , Rangi n.k KIBOKO Paints, imefanya semina maalum kwa Mafundi Ujenzi zaidi ya 125 Mkoani Kahama kwa lengo la kuwaelezea mabadiliko na maboresho makubwa waliyoyafanya kwenye bidhaa zao mbalimbali hasahasa Rangi za KIBOKO pamoja na kuitambulisha bidhaa yao mpya ya KIBOKO WALL PUTTY kwa mafundi hao.
Akizungumza baada ya Semina iyo iliyofanyika Jumamosi ya Julai , 27 , 2024 Mjini Kahama Afisa Masoko Mkuu wa Makampuni ya KIBOKO Bwn. Erhard Mlyansi amesema wamefika KAHAMA ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na Mafundi nchi nzima kwa ajili ya kupeana taarifa na mrejesho kuhusu bidhaa za KIBOKO
" Tumepata mwitikio mkubwa wa Mafundi wa Kahama tumebadilishana mawazo na kupeana elimu mbalimbali kuhusiana na bidhaa za KIBOKO naamini baada ya hapa watakua mabalozi wazuri wa bidhaa zetu zenye ubora wa hali ya juu "
Aidha Bwn. Mlyansi amewasihi Watanzania kupenda bidhaa za ndani , maana ndizo zitakazochangia kukua kwa uchumi wetu na kutoa ajira kwa wana jamii huko viwandani zinapotengenezwa , kama ilivyo Kampuni ya KIBOKO ambayo mmiliki wake ni Mtanzania na Bidhaa zake zote zinazalishwa hapa nchini .
Akizungumza kwa niaba ya Mafundi Mwenyekiti wa Chama cha Mafundi Ujenzi Kahama ( CHAMAUKA ) Bwn. Baraka Majengo ameipongeza Kampuni ya KIBOKO kwa semina hii kwa maana wameweza kujifunza mengi kuhusiana na Bidhaa zao mpya na za zamani , Aidha ameishukuru kampuni ya KIBOKO kwa kuchangia Fedha kwa ajili ya mfuko wa CHAMAUKA.
Akiizungumzia KIBOKO WALL PUTTY amesema
"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni " .
No comments