MAFUNDI KIGAMBONI WASHUHUDIA MAAJABU YA RANGI NA WALL PUTTY ZA KIBOKO
PICHA YA PAMOJA : Baadhi ya Mafundi kutoka Kigamboni Jijini Dar Es Salaam katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Utengenezaji , Uuzaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY yenye ubora wa hali ya juu kwa mafundi hawa , Mapema leo Julai , 06 , 2024 Katika Ukumbi wa Arena - Kigamboni .
Leo , Julai 6, 2024 akizungumza baada ya Semina hiyo , Bwn. Hamidu Satara ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema
" Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung'ara hata kama haujapigwa rangi. " amesema Bw. Hamidu
Sambamba na hilo , Mafundi wamepata nafasi ya kujionea maboresho makubwa ambayo kampuni ya Kiboko imeyafanya katika rangi zake , ambazo kwa sasa ni bora ukilinganisha na zilivyokua miaka kadhaa iliyopita , mafundi wamepata nafasi ya kuilinganisha rangi ya KIBOKO na Rangi za makampuni mengine kwa kuipiga kwenye ubao ambapo matokea yaliyopatikana baada ya muda mfupi yameonesha dhairi kwamba rangi ya KIBOKO imeboreshwa kwa kiwango kikubwa .
"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni, lakini pia rangi yao ni nzuri sana " amesema.
.
No comments