PPRA WAJA NA FURSA KIBAO SABASABA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeanza kufanya kazi kwa mujibu wa sheria mpya ya manunuzi, ambapo pamoja na mambo mengine inaelekeza zabuni zote za Shilingi bilioni 50 na chini ya hapo zitolewe kwa wazawa.
Mkurugenzi wa Utafiti, Maendeleo, na Ubunifu wa PPRA, Mhandisi Masunya Nashon, ameyasema hayo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa 48 ya Dar es Salaam na kuelezea kuwa kuanzia Oktoba 1, 2023, sheria mpya ya manunuzi namba 10 ya mwaka 2023 na vifungu vyake kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 518 la Juni 2024, ilianza kutumika jambo ambalo limeongeza wigo wa wananchi na maeneo hayo.
Ameitaja sheria mpya ya Mfumo wa Taifa wa Ununuzi wa Kielektroniki Tanzania (NEST) ambao ni mfumo wa kielektroniki na amesema sheria hiyo mpya imekuja kwa kuwaangalia zaidi wazawa kwa kutoa upendeleo kuanzia kifungu namba 56 hadi 64 sheria hiyo inasema kuwapa upendeleo makundi matatu lile la vijana,wanawake, wazee na watu wenye mahitaji maalum.Sheria hiyo imeelekeza kila taasisi nunuzi Serikali itenge asilimia 30 ya bajeti kwa ajili ya kuyawezesha makundi hayo kushiriki katika zabuni za serikali na hivyo Serikali kupitia PPRA inaanza kutoa mafunzo kuwajengea uwezo juu ya mfumo mpya wa ununuzi ya umma kwa mfumo wa kielektoniki, kanuni wa sheria za manunuzi.
Mfumo huo umeanza Oktoba 1 mwaka jana tayari taasisi nunuzi 1147 na wazabuni zaidi ya 22000 ambao tayari wameshajiandikisha katika mfumo,na sheria mpya inatoa upendeleo kwa bidhaa na malighafi zinazozalishwa nchini kwa kuzijengea uwezo taasisi za manunuzi kupitia sheria mpya na kanuni mpya na NEST.
No comments