Breaking News

BIDHAA ZA NGOZI ZA DIT ZAWAVUTIA WENGI SABA SABA.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) Prof. Ezekiel Amri ( aliyevaa koti ) akiziangalia baadhi ya Bidhaa za ngozi kama vile viatu, mikanda , mikoba n.k zilizotengenezwa na wanafunzi wa DIT Kampasi ya Mwanza mapema leo hii Julai , 04 , 2024 alipotembelea banda la DIT lililopo katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar Es Salaam.





PICHA TOFAUTI TOFAUTI : Wageni mbalimbali waliolitembelea banda la DIT lililopo Kwenye Maonesho ya Sabasaba wakizitazama na kununua bidhaa za Ngozi hasa viatu vilivyotengenezwa DIT Kampasi ya Mwanza , pembezeno mwao ( waliovaa sare ) ni Wataalam wa Uchakataji wa Bidhaa za Ngozi kutoka DIT Kampasi ya Mwanza Ramadhan Khalfan Buthu na Azaria Chongeri.

Clement Mahemba Mkazi wa Ubungo Jijini Dar Es Salaam akijaribu viatu baada ya kuvinunua katika Banda la DIT lililopo Maonesho ya Sabasaba , kulia ni Mtaalam wa Uchakataji wa Bidhaa za Ngozi kutoka DIT Kampasi ya Mwanza Ramadhan Khalfan Buthu.

Na Mwandishi Wetu.

Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) inashiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Temeke Jijini Dar Es Salaam , na DIT imekuja na Bunifu mbalimbali zilizobuniwa na Wanafunzi wa Taasisi hiyo nyingine zikitoka kwenye Kampuni Tanzu ya Taasisi hiyo maarufu kama DIT COMPANY. 

Bidhaa zilizowavutia watu wengi waliotembelea Banda la DIT ni bidhaa za Ngozi kama vile Viatu, mikanda n k ambazo zinatengenezwa na DIT Kampasi ya Mwanza . 

Clement Mahemba Mkazi wa Ubungo Dar Es Salaam ni miongoni mwa watu waliopata bahati ya kutembelea Banda la DIT Leo Julai 04 , 2024 na kununua viatu akizungumza na Mwandishi Wetu na kuulizwa kwanini ameamua kununua viatu vya DIT Clement amesema kwamba sababu kuu ni BEI na UBORA. 

" Nimekua nkisikia kuhusu bidhaa za Ngozi za DIT hasa hasa Viatu na Mikanda na baada ya kufika katika Maonesho haya nikaona wana Banda lao ndipo nikaingia na kununua pea kadhaa za Viatu , kwakweli viatu vyao ni vigumu (Ngozi asilia ) na Bei nafuu ". amesema 

Aidha Clement amewasihi Wazazi na Vijana hasa waliomaliza kidato cha 4 na 6 waweze kujiunga na DIT Kampasi ya Mwanza ili kujipatia ujuzi wa Kutengeneza bidhaa kama hizi maana itawapa mwanya mpana wa kujiajiri na kuajirika katika makampuni mbalimbali na hata Serikalini.

No comments