TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Diwani wa kata ya Goweko Mhe. Shaban Katalambula iliyotolewa na TCB kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji iliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Wananchi wakishusha cement iliyotolewa na Tanzania Commercial bank kwaajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati
TCB imeunga mkono jitihada zilizoanzishwa na wanakijiji wa kata hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Kwa muda mrefu wananchi wa kata ya Goweko wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za afya, hivyo kwa msaada toka benki ya TCB itawezesha kutatua changamoto hizo kwa wananchi hao.
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania Commercial bank TCB inaendelea kuwakaribu zaidi na watanzania ambao ndio wateja wake wakubwa, Iimeunga mkono juhudi za Wananchi wa kata ya Goweko kwakukabidhi msaada wa mifuko 100 ya Saruji.
Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Benk ya TCB, Bi Chichi Banda alisema kuwa Tanzania Commercial Bank kama ilivyokawaida yake imeguswa na imefanya maana inaamini hawa wananchi ndio wateja wa benki.
“leo tunakabidhi msaada wa mifuko 100 hapa kwaajili yakukamilisha ujenzi wa kituo cha afya lakini pia hatukuishia hapa tumekabidhi mifuko 100 mingine kwa Diwani wa Kata ya kiburugwa Mbagala Dar es salaam kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha polisi cha kata hiyo".
Pia tukatambua umuhimu wa sekta ya elimu nako tumeweza kutoa mifuko 150 ya saruji katika Shule ya Msingi Ikamba iliyoko wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwaajili yakufanya maboresho ya madarasa.
“tunawapongeza sana wakazi wa hapa kwakuona kuwa swala la afya sio la serikali pekeyake hivyo sisi kama TCB tumeguswa sana tumeona tuje hapa kusaidiana na wananchi kwa hali na mali kwani nyinyi ni sehemu yetu na sisi ni sehemu yenu,"
Tanzania Commercial Bank ni benki pekee nchini yenye mtandao mpana wamatawi na mawakala nchi nzima hivyo niwasihi ndugu wananchi muitumie Benki ya TCB kwani inabidhaa bora na rafiki.
No comments