Kampuni ya LG yabainisha mkakakati wa mwaka 2023 ulioko katika mpango wake wa maendeleo endelevu kufikia mwaka 2030.
Mkakati huo unajumuisha uvumbuzi unaolenga mahitaji ya wateja kujenga maisha bora kwa wote, na kujali mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji bwana Cho, katika ‘LG World Premiere’, alibainisha Dira ya Uvumbuzi iliyoundwa kufanya maisha ya wateja kuwa bora.
Mkurugenzi Mtendaji vile vile alitaja ahadi ya kampuni ya kuongeza upatikanaji wa bidhaa na huduma za LG kuhakikisha urahisi wa kutumIwa na walemavu na wazee.
Kampuni ya LG inatazamia kutumia 100% ya nishati mbadala kufikia mwaka 2025, kupunguza gesi ya ukaa na kuhamasisha mabadiliko ya soko kupitia katika uvumbuzi wake.
************************ NA MWANDISHI WETU***************
Tarehe 9 Januari 2023 Nairobi, Kenya. Kampuni ya LG Electronic imetangaza mkakati wake wa mwaka 2023 wenye lengo la kujenga ubunifu kwaajili ya maisha bora na kuhakikisha maisha endelevu kwa wote.
Ikiwa inatumia kauli mbiu yake ya "Life is Good" mpango huu uliwekwa bayana na Mkurugenzi Mtendaji wa LG bwana Wliiam Cho wakati wa mkutano mkuu wa LG na Vyombo vya habari uliofanyika kando kando ya maonyesho ya CES 2023 yanayoendelea.
Inaonyesha upatikanaji madhubiti wa uvumbuzi ambao unalenga mahitaji ya wateja kwa dhumuni la kujenga maisha bora kwa kila mmoja, na kujali mazingira, mpango ambao umeambatishwa katika mkakati wa 2023 ESG wenye jina la better Life life, na mpango kazi wake uitwao Better Plan ambao unalenga katika kujenga upatikanaji, urahisi wa bidhaa na huduma kutumiwa na watu wenye walemavu na wazee.
Akiongea wakati alipokuwa akitangaza maono ya kampuni. Bwana William Cho alisisitiza utayari wa kampuni wa kuchukua changamoto mpya katika mwaka 2023 na kuendelea bila kujali hali yoyote, akigusia kwamba kampuni ya LG imekuwa inafahamu na kuamini kwa dhati kwamba jibu liko kwa mteja. Mwanzo na mwisho wa ubunifu wote ni wateja wetu, na ni kwa kupitia ubunifu huu ndipo tunapolenga kuweka tabasamu katika nyuso zao.
WATU
Kuwapatia wateja wake thamani mpya, Bwana Cho aligusia kuhusu ubunifu mkubwa ujao unaolenga wateja katika bidhaa zake za umeme za majumbani kama vile LG OLED ambayo imebadilisha moja kwa moja namna ambavyo wateja walivyokuwa wanangalia televisheni zao.Alibainisha kwamba kampuni inafanya kazi na washirika wake kutambulisha aina mbalimbali za huduma kupitia LG TVs, ikiwemo mfumo wa elimu kwa njia ya mtandao MasterClass, programu ya mazoezi MaxPro na huduma za metaverse Sansar ambazo zitapanua uzoefu wa wateja na kuwezesha watumiaji wa TV kupata uzoefu mpya katika uangaliaji. Wakati ambapo inasherehekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa, bidhaa za LG OLED inaendelea kuweka viwango vipya vya ubora katika sekta kwa ubora wa picha na uzoefu wa wateja ambao haujawahi kutokea.
Kwa kuongezea, Bwana Cho vile vile aliongelea kuhusu LG Think UP,aina mpya ya vifaa vya nyumbani vinavyoendelea kubadilika; vinavyotoa fursa ya kipekee vinavyoweza kuboreshwa na kubadilishwa kuendana na mahitaji ya mtumiaji. Orodha ya kipekee ya bidhaa zinajumuisha bidhaa za kimapinduzi kama Jokofu la LG lenye MoodUP™, ambayo inaweza kubadili rangi kuendana na mahitaji ya mtumiaji, anavyojisikia au kuendana na mapambo ya jiko.
Akiwa anasisitiza malengo ya kampuni ya kutengeneza maisha bora ya baadae kwa wote, bwana Cho alisisitiza utayari wa kampuni ya LG kama shirikja lenye uwajibikaji kwa jamii kuweza kufikia maendeleo endelevu. Alitaja ahadi ya kampuniya kuongeza upatikanaji na urahisi wa kutumia bidhaa na huduma za LG kwa walemavu na wazee. Ahadi hii kama ambavyo inaongozwa na maoni kutoka kwenye Kikundi cha Ushauri cha Walemavu cha LG (‘Disabled Advisory Group) -ambacho kinafanyakazi tangu 2021 ambacho kina wajumbe wenye uwezo tofauti tofauti na wataalamu wa ufikivu - kampuni inaendelea kutambulisha bidhaa zisizo na uzuizi ambazozinaweza kutumiwa na watu wote kwa urahisi.
Dhumuni letu ni kuondoa vizuizi katika hatua zote za matumizi ya mteja. Hatua hii itajumuisha kutengeneza mwongozo wa bidhaa ambao unajumuisha sauti na lugha ya ishara, kusambaza stika za braille kwajili ya watu wenye ulemavu wa macho, na lugha ya ishara kwaajili ya kuendeshea vifaa miongoni mwa mengine." alisema Cho.
Katika kukamilisha jambo hili hivi sasa kampuni ya LG inaendesha mashindano ya Teknolojia ya Habari ulimwenguni (Global IT Challenge) kwa vijana wenye ulemavu (GITC) ambayo tangu mwaka 2011 imewawezesha zaidi ya vijana 4,000 kujenga ujuzi katika teknolojia kuondoa mgawanyo ya kidigitali kwa watu wenye ulemavu.
MAZINGIRA
Kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu na sayari, kampuni ya LG Electronics imebainisha mpango wake wa kuweka watu na sayari katika nafasi ya kwanza ambalo liko katika moyo wa mpango wa Maisha Bora 2030 (Better Life Plan 2030) Mfumo wa kimataifa wa LG kwaajili ya mazingira, jamii na utawala ambayo inaeleza majukumu ya msingi ya ESG na usimamizi wa ESG Led Katika agenda ya mazingira, LG ina lengo la kutumia tani 600,000 ya plastiki iliyorejeshwa kufikia mwaka 2030 katika mchakato wake wa uzalishaji, jambo ambalo linathibitisha utayari wake kuongoza njia kuelekea katika mazingira endelevu na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa zaidi ya maiaka 7 ijayo kampuni ya LG imepanga kukusanya na kuchakata tani milioni 4.5 za taka. Katika hali hiyo hiyo, Wataalamu wa LG wanalenga kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia 20 katika bidhaa zake 7 kubwa kupitia matumizi yenye ufanisi ya nishati, hata wakati ambapo inalenga kukamilisha mabadiliko yake kuelekea katika nishati mbadala kufikia 2050.
Sambamba na hili, Mkurugenzi Mtendaji alitangaza kuendelea kuunga mkono tuzo za LIFE’S GOOD AWARD, shidano la ubunifu ililowekwa na kampuni kwa lengo la kutangaza maono yake ya Life IS Good na kuwawezesha wabunivu wenye hamu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya watu na sayari yetu.
WAKATI UJAO
Akielekea katika wakati ujao Mkurugenzi Cho alidokeza kuhusu sekta ya vyombo vya usafiri, akieleza kwamba kampuni imeungana na baadhi ya makampuni maarufu ya vyombo vya usafiri, kutumia ufahamu wa wateja wake kutoka kwenye watumiaji wa vifaa vya umeme, teknolojia ya kiwango cha juu na maeneo mbalimbali ya utaalamu kuboesha uzoefu wa kusafiri ndani ya gari.Hatua hii imepelekea kampuni ya LG kuwa moja kati ya kiwanda cha vifaa vya magari cha kutumainiwa kwa biashara yake ya bidha ya vifaa vya magari, hata wakati ambapo inapanua biashara yake kujumuisha maeneo mapya kama vile chaji za (EV) za magari ya umeme, Vifaa vya kidigitali vya kiafya na huduma ya maudhui kwaajili ya mfumo wa webOS.
Wakati huo huo, kampuni inaongeza uwekezaji katika teknolojia ya msingi ya siku zijazo, ikiwemo AI na 6G pamoja na kushirikiana na wataalamu chipikizi wa teknolojia kupitia LG, NOVA, (LG North American Innovation Center).
Zaidi ya sekta ya usafiri, Cho vile vile alibainisha lengo la kampuni la kutoa uzoefu wa kwanza, wa kipekee, na mpya katika bidhaa na huduma zake zote kwa dhumuni la kuleta maisha bora kwa wote. Kwa lengo la kupanua uzoefu wa wateja katika maeneo mbaimbali, kampuni vile vile inaendesha programu mbalimbali za ndani kukuza wavumbuzi. kuhamasisha wafanyakazi wa LG kukubaliana kwa ujasiri na changamoto mpya.
No comments