MHE. MTEMVU AIPONGEZA KAMPUNI YA HERITAGE DRINKING WATER KWA KUISADIA SERIKALI , UZINDUZI WA KITUO CHA KUUZA MAJI KIMARA TERMINAL
Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe. Issa Mtemvu ( kulia ) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya maji safi na salama ya HERITAGE DRINKING WATER katika kituo cha Magari ya Mwendokasi Kimara Mwisho Jijini Dar Es Salaam , Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dkt. Edwinus Lyaya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya HERITAGE DRINKING WATER Dkt. Edwinus Lyaya akitoa maelezo kuhusu teknolojia inayotumika kusafisha maji hayo , pamoja na taratibu mbalimbali ambazo kampuni iyo imefuata mpaka kufikia hatua ya kutoa huduma iyo kwa jamii, pembeni ni baadhi ya wafanyakazi wa HERITAGE DRINKING WATER.
Baadhi ya wasafiri na wananchi wa Kimara Mwisho wakishuhudia uzinduzi wa Huduma ya maji safi na salama ya HERITAGE , yatakayouzwa kwa Shilingi 200 / Lita saa 24, katika kituo hicho.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Kitanzania ya Uuzaji wa maji safi na Salama kwa bei nafuu ya Tsh. 200 / Litre ya HERITAGE DRINKING WATER Leo Januari 7, 2023 imefungua kituo kipya cha kuuza maji ndani ya Stendi ya Mwendokasi ya Kimara Mwisho Jijini Dar Es Salaam kituo kilichozinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe. Issa Mtemvu
Akizungumzabaada ya Uzinduzi huo Mhe. Mtemvu amempongeza Bwn. Edwinus Lyaya ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Heritage Drinking Water , kwa Ubunifu huu na kuahidi kuunga mkono kampuni hii ya Kitanzania kuhakikisha inaendelea kutoa huduma hii ya Maji safi na salama ambaye kauli mbiu yake ni " TUNZA PESA OKOA MAZINGIRA " " Hakika HERITAGE DRINKING WATER mnafanya mambo makubwa na hatuna budi kuwaunga mkono , nimeona hapa bei za maji yenu Shilingi 200 kwa lita moja ni bei ndogo sana kulinganisha na ubora wa maji mnayoyatoa hakika inabdi tuwaunge mkono muweze kuwafikia watanzania wengi zaidi Ndani na hata nje ya Jiji la Dar Es Salaam ili kila mtanzania aweze kuokoa pesa huku akitunza mazingira kama kauli mbiu yenu inavyosema , pamoja na hilo mnatoa ajira, mimi ni mbunge nayetokana na CCM na ilani ya Chama chetu ni kutoa ajira MILIONI 8 ndani ya miaka mitano kwahiyo nikupongeze maana mnamsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutoa ajira, lakini mefurahi kwa kusikia maji yenu yamethibishwa na TBS ni jambo muhimu sana " AlimaliziaNao baadhi ya wakazi wa Kimara mwisho ambao ni Elizabeth Robert na Abdal Sulleiman Khamis wameipongeza kampuni ya HERITAGE DRINKING WATER kwa kuwaletea huduma hii , maana itawasaidia sana.
No comments