Breaking News

TBS WAFANYA MKUTANO MAALUM NA WAZALISHAJI , WAINGIZAJI NA WASAMBAZAJI WA BIDHAA ZA MABATI , NONDO NA STEELS

 Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania ( TBS )  Dkt. Candida Shirima akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Maalum na Wadau ambao ni Wazalishaji , Waingizaji , na Wasambazaji wa Bidhaa za Mabati , Koili za Kutengeneza Mabati , Nondo , na Steel Section ambazo zinahusisha Square pipe , Round pipes na Flat bars . Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya TBS Jijini Dar Es Salaam.
                                       ********************

Na Adery Masta.

 Leo Januari 24, 2023 Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo Tanzania wameendesha Mkutano Maalum na Wadau ambao ni Wazalishaji , Waingizaji , na Wasambazaji wa Bidhaa za Mabati , Koili za Kutengeneza Mabati , Nondo , na Steel Section ambazo zinahusisha Square Pipe , Round pipes na Flat bars , Kikao ambacho Wataalam kutoka TBS wakishirikiana na Wataalam kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania watatoa Mada za Msingi ambao zitawajengea wadau hawa uelewa kuhusiana na namna bora ya kuzingatia Viwango vya Ubora wa bidhaa wanazohusika nazo , Ikiwa ni Azma ya Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imelenga kujenga uchumi imara , Shindani , Wenye nguvu na Endelevu ambapo katika kuunga mkono Jitihada hizo TBS inawajibika kikamilifu katika kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazoingizwa toka nje ya nchi zinakidhi matakwa ya Viwango ili kukuza Uchumi wa Nchi .

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi TBS Bi. Candida Shirima amewapongeza Wadau ambao ni Wazalishaji , Waingizaji , na Wasambazaji wa Bidhaa za Mabati , Koili za Kutengeneza Mabati , Nondo , na Steel Section ambazo zinahusisha Square Pipe , Round pipes na Flat bars kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo 

" Ndugu Washiriki Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) limeandaa mkutano huu kwa ajili ya kukuza uelewa wenu kuhusu matakwa ya Sheria ya Viwango Sura ya 130 ambayo ndiyo sheria iliyoanzisha TBS na iliyoipa TBS haya majukumu ya Uthibiti lakini pia matakwa ya kanuni mbalimbali zilizotungwa chini ya hii Sheria ya Viwango , pamoja na Sheria ya Wakala wa Vipimo Nchini ".





No comments