USAID KIZAZI HODARI TUMAINI JIPYA KWA JAMII ZA WAATHIRIKA WA UKIMWI
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima (wa pili kushoto) akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Deloitte Consulting, Zahra Nensi baada ya kuzindua mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu KKKT, Mhandisi Robert Kitundu. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima akibonyeza kitufe kuzindua mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini, Kate Somvongsiri akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na USAID.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Mradi wa Kizazi Hodari Kanda ya Kusini, Dorothy Matoyo baada ya kuzindua mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Deloitte Consulting, Zahra Nensi. Mradi huo unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Mkurugenzi Mkazi wa Deloitte Consulting Limited, Zahra Nensi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Mkurugenzi wa Mradi wa Kizazi Hodari, Dorothy Matoyo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Mkuu wa Kanisa la KKKT, Askofu Dk. Fredrick Shoo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Baadhi ya Viongozi wa dini wakihudhuria wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Baadhi ya wahudhuriaji wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Jamii na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima ameagiza utekelezaji wa mradi wa Kizazi Hodari unaowalenga kuimarisha afya, ustawi na ulinzi kwa Watoto na vijana balehe wanaoishi katika mazingira hatarishi yenye Kasi kubwa ya maambukizi ya VVU.
Mradi wa Kizazi Hodari utatekelezwa kwa miaka mitano chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) na unawalenga watoto balehe wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 17.
Watekelezaji wa mradi huo ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Shirika la Deloitte na Shirika la kidini la KKKT
Taasisi ya Deloitte ikisimamia mikoa mitano ya Kanda ya Kusini ya; Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe huku Kanisa la KKKT likisimamia mikoa Saba ya Kanda ya Kaskazini ya; Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Singida na Dodoma.
Akizungumza jana katika uzinduzi wa mradi huo, Dk Gwajima alisema mbali na mambo yaliyoainishwa katika mradi huo utakaotekelezwa kwenye mikoa 12 nchini, ni muhimu mradi huo ukajihusisha na utoaji wa elimu sahihi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
“Ni vema afua zifuatazo zikawekwa katika mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa Kizazi Hodari ni kutoa elimu sahihi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na kuendeleza programu za kuwaandaa wavulana kuwa wanaume bora wajao,” alisema.
Akielezea kuhusu mradi huo, Dk Gwajima alisema jumla ya watoto yatima na kaya 138,944 zitafikiwa na mradi huo ambao unalenga katika kuimarisha afya, ustawi na ulinzi kwa watoto na vijana balehe wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Deloitte, Zahra Nensi alisema mradi huo unalenga katika kuongeza wigo wa kuwatambua watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na kuwaunganisha karika huduma za afya ili kufubaza VVU.
“Kuongeza upatikanaji wa huduma za kuzuia maambukizi, kuzuia ukatili na huduma za mwitikio kwa watoto yatima na vijana,” alisema.
Pia alisema lengo jingine ni kukuza uchumi kwa ajili ya mabinti balehe na walezi wa watoto yatima na waishio mazingira hatarishi.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Kate Msomvongsiri amesema hadi mwisho wa mradi huo inategemewa utakuwa umeajiri na kuwapatia huduma mbalimbali walau kwa asilimia 90 ya watoto na vijana hao.
Alisema vijana hao ni hasa kutoka kwenye vituo vya afya vinavyohudumiwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR).
No comments