TAASISI YA UWEZESHAJI WAJASIAMALI YA OPEN MIND AND THOUGHTS ORGANIZATION (OMTO) YALETA NEEMA KWA WATANZANIA
Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kulia),
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Mkurugenzi
wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO),
Anna Haule wakionyesha kwa pamoja Mkoba wa nyaraka za Taasisi ya OMTO katika
uzinduzi wa taasisi hiyo yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake,
wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo
ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya
Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (kulia) akizungumza na
wajasiriamali pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa taasisi
hiyo yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na
watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa
Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Raisi wa Vicoba Endelevu,
Devotha Likokola.
Mwakilishi
wa Ofisi ya serikali ya mtaa ya Kitunda, Mwanahawa Zinga akizungumza katika hafla ya uzinduzi
wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)
iliyochini ya Vicoba endelevu uliofanyika ofisini mwa taasisi hiyo Kitunda
jijini Dar es Salaam. Wapili kulia
ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Haule, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Guru Planet, Nickson Martin na Raisi wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola.
Raisi
wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola akizungumza na wajasiriamali pamoja na
wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji
Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) yenye lengo la
kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu
kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda
jijini Dar es Salaam. Vicoba Endelevu ni mwamvuli wa taasisi ya OMTO.
Baadhi ya Wanachama wa Taasisi ya Uwezeshaji
Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) pamoja na vikundi
vingine vilivyopo chini ya Vicoba endelevu wakisikiliza kwa makini mada
zinazoendelea wakati wa Uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wageni Waalikwa wakizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya
Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (wa pili kushoto)
akiitambulisha Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika
ofisini mwa taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam.
Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kushoto),
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule, Mkurugenzi wa taasisi ya Data Sustainable
Development Organization (Data), Sihaba Madenge na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Women Movement and Effort Organization (Wmeo), Anna Basita wakitumbuiza wakati
wa hafla ya uzinduzi wa taasisi OMTO yenye
lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye
ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo
Kitunda jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto wa wanachama wa OMTO
wakitumbuiza wakati wa Uzinduzi wa taasisi hiyo.
Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kulia)
na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule wakikata keki kuashiria uzinduzi wa Taasisis ya
OMTO uliofanyika ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es
Salaam.
Raisi
wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kushoto) akimlisha keki Mgeni rasmi Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin katika hafla hiyo.
Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and
Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya
Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (kushoto) akikabidhi
keki kuashiria shukrani kwa Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru
Planet, Nickson Martin katika hafla hiyo. Kulia ni Raisi wa Vicoba Endelevu,
Mh. Devotha Likokola.
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Guru Planet, Nickson Martin akikata utepe katika uzinduzi wa Taasisi ya
Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) hiyo yenye
lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye
ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo
Kitunda jijini Dar es Salaam. Kulia ni Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh.
Devotha Likokola na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Haule.
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Guru Planet, Nickson Martin akizungumza katika hafla hiyo.
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Uwezeshaji
Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) imesajiliwa rasmi tarehe 5/8/2019 ikiwa na
ruhusa ya kufanya kazi ndani ya Tanzania na bara kwa kuzingatia lengo kuu la
serikali la kuboresha maisha kwa kila mtanzania.
Taasisi hii imeona umuhimu wa
kusaidiana na serikali na kuhakikisha lengo kuu la serikali kuwa na Tanzania ya
viwanda linatimia.
Akizungumza Mkurugenzi wa OMTO,
Anna Haule "Taasisi hii ina malengo yafuatayo kuhamasisha wananchi
kushiriki katika shughuli za kijamii, kushawishi jamii kujiunga katika vikundi
vya ujasiriamali, kuhasisha jamii kuwa na tabia ya kuweka akiba ili kukuza
mitaji na kufanya biashara endelevu pamoja na kujenga uwezo kiuchumi kwa
wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiamali".
Alisema Mkurugenzi.
Taasisi kwa sasa inavikundi 15
kwa hapa Dar es Salaam na mikoni yenye jumla ya wanachama 600 ikiwemo wanawake
ni 85% na wanaume ni 15%.
Kwa elimu wanayoipata ya kuweka
akiba na kufanya ujasiamali wa pamoja baadhi ya vikundi tayari wameshaanza
kufanya ujasiriamalikwa utengenezaji wa batiki, sabuni za maji na pilipili ya
embe malengo ni kuanzisha kilimo (green house), ufugaji wa kuku, samaki na
nyuki.
Nae Raisi wa Vicoba Endelevu,
Mhe. Devotha Likokola akizungumza "Miongoni mwa fursa zilizopo ni kuwa
pamoja katika kufanya ujasiamali ili kuwekeza kutimiza malengo ya nchi yetu ya
Tanzania ya viwanda na imani kubwa ni kufikia kuwa na viwanda vidogo vidogo na
kwa baadae kuwa na viwanda vikubwa". Alisema Raisi.
HABARI PICHA KATIKA MATUKIO
No comments