RC MAKONDA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YA MWENDOKASI MBAGALA NA KUTANGAZA NEEMA KWA WAKAZI WA MBAGALA
Kilio cha Wakazi wa Mbagala juu ya Changamoto ya Usafiri kilichokuwa kikipelekea abiria kugombea magari kwa mtindo wa kuingilia madirishani, kukaa kwenye foleni, Wizi wa mikoba na Simu kinategemewa kuisha hivi karibuni kufuatia ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi unaoendelea ambapo leo Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe.
Paul Makonda ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo na kueleza kuridhishwa na juhudi za mkandarasi huyo.
RC Makonda amesema ujenzi wa Barabara hiyo unagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 200 na itakuwa na urefu wa Km 20.3 ikianzia Mbagala Rangi tatu kuelekea Kariakoo na Posta mbapo pia itakuwa na Fly Over Mbili.
Aidha RC MAKONDA amesema ujenzi wa barabara hiyo utaenda sambamba na kuunganisha Kipande cha Kutokea Magomeni kupitia kigogo, Chang'ombe hadi Round about ya Mgulani JKT.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema Wilaya ya Temeke imepata neema kubwa ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa Km 80 chini ya DMDP kwenye kata Sita ambazo tayari zimekamilika jambo lililopunguza usumbufu Kwa wananchi wa Temeke.
Katika ziara hiyo RC Makonda pia ametembelea Ujenzi wa Uwanja wa Mpira na Basketball wwnye thamani ya Milioni 768 unaojengwa kata ya Makangarawe Wenye uwezo wa kuchukuwa watu 800 hadi 1,000 ambao unatrajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu na kuanza kuopandwa nyasi ili utumike mwezi April mwakani.
Hata hivyo RC Makonda ametembelea ujenzi wa Soko la Kisasa la Makangarawe lenye uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara 300 kwa wakati mmoja ambapo amewaomba Wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali.
TUKUTANE SITE 2019.
No comments