KAMPUNI YA VISA YAZINDUA KAMPENI YA KUFANYA MALIPO KWA NJIA YA VISA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA SIKUKUU YA KRISMASI,
Balozi wa Kampuni ya VISA ambepia ni Msanii anaeunda kundu la Navy Kenzo Aika Marealle (kushoto) akiwa na moja ya wateja wanatumia kadi ya VISA kufanya malipo wakati wa uzinduzi wa kampeni inayoitwa 'Sherekea na Visa' ambayo imezinduliwa jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Kampuni ya Visa wakipiga picha na Mteja wakati wa uzinduzi huo
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleve wanaounda kundi la NAVY KENZO Emmanuel Mkono pamoja na Aika Marealle ambao ni Mabalozi wa Visa, wakipiga picha na mmoja ya wateja anetumia Visa kufanya manunuzi.
KAMPUNI ya Teknolojia ya malipo ulimwenguni(VISA) imezindua kampeni katika msimu huu wa sikukuu Watanzania wenye kadi ya VISA wataweza kufanya malipo yao ya manunuzi bila kutumia fedha taslimu ambapo pia watakaofanya manunuzi watapata zawadi mbalimbali .
Kampeni hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Kampuni ya VISA imewahimiza wanunuaji bidhaa katika Jiji hilo kwenda katika maduka makubwa kwa ajili ya kufanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Meneja wa VISA nchini Tanzania Olever Njoroge amesema itaendelea hadi Desemba 22 mwaka huu ambapo wateja ambao watafanya malipo kwa kutumia kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.
Amesema kampeni hiyo ambayo wameizundua kwa ajili ya wateja wenye Kadi za VISA ina malengo ya kuhamasisha utumiaji wa kadi ya VISA au VISA kwenye simu wakati wa manunuzi katika maduka ya Mliman City Mall, Shoppers Masaki na Shopers Mikochoni.
"Kampeni hii ina malengo ya kukuza utumiaji wa kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi, Tunawahamiza wateja wetu wa Tanzania kufanya malipo kwa njia ya Visa ambapo itawapa urahisi na usalama kipindi cha manunuzi wakati huu wa Krismasi,"amesema Njoroge.
Ameongeza kuwa wanaileta VISA kwa Watanzania wakizingatia faida katika kufanya manunuzi yao kwa kutumia kadi ya VISA au VISA kwenye simu ya mkononi ma kwamba wanajivua kwamba sasa Watanzania wapo huru kutumia njia mpya za malipo bila kuwa na fedha mkononi.
Amefafanua kuwa kampeni hiyo ya Krismasi na VISA itawapa wanunuzi fursa ya kuchagua Zawadi za aina gani kumpatia mteja wao kwa njia rahisi na salama wanaponunua bidhaa kwenye Mall.
Amesema mapema mwaka huu VISA kwa kushirikiana na benki 15 za Tanzania wazilizindua VISA kwa njia ya simu ya mkononi ."VISA kwa kushirikiana kwa njia ya simu ya mkononi ni suluhisho la malipo ya dijiti ambayo inaruhusu watumiaji kutumia fedha kwa kila mmoja bila kulipa ada ya ununuzi.
"Kutumia huduma hiyo ,mtu anapaswa kupakua app ya benki yake, atafute VISA kwenye app na alipe bidhaa na huduma kwa kuiscan code ya QR au kwa kutumia nambari ya USSD,"amesema huku akielezea wazi Watanzania wengi wamekuwa na muamko mkubwa wa kutumia VISA kufanya malipo katika manunuzi mbalimbali.
About Visa Inc.
Visa Inc. (NYSE: V) is the world’s leader in digital payments. Our mission is to connect the world through the most innovative, reliable and secure payment network - enabling individuals, businesses and economies to thrive. Our advanced global processing network, VisaNet, provides secure and reliable payments around the world, and is capable of handling more than 65,000 transaction messages a second. The company’s relentless focus on innovation is a catalyst for the rapid growth of digital commerce on any device for everyone, everywhere. As the world moves from analog to digital, Visa is applying our brand, products, people, network and scale to reshape the future of commerce. For more information, visit About Visa,visa.com/blog and @VisaNews.
For media queries, contact:
Emily Kaiga
Visa Corporate Communications
Myoma Kapya
Hill+ Knowlton Strategies
No comments