WAITARA NA KUMBILAMOTO WAPOKELEWA KWA KISHINDO CCM
Wanachama wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) wakimpokea kwa shangwe Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,
Mwita Waitara (wapili kushoto) baada ya kuwasili katika Mkutano wa ndani wa
chama hicho uliofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.Waitara alikuwa Mbunge wa Ukonga kwa Tiketi ya Chadema sasa amejiuzulu na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akisalimiana
na Diwani wa kata ya Chanika, Ojambi Masaburi wakati akiwasili katika mkutano
wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye ajenda ya kuwapokea rasmi Waitara
na Kumbilamoto pamoja na Viongozi na wanachama wengine baada ya kuhama kutoka
vyama vya upinzani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.Mapokezi hayo yamefanyika
katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa
kata ya Kivule, Gisiri Anthony (alivevaa shati jeupe) akipokelewa na akina mama
wa Chama Cha Mapinduzi katika kikao cha ndani cha Chama hicho kilichofanyika
katika kata Pugu jijini Dar es Salaam jana.Gisiri alikuwa ni Mwenyekiti wa Kata
ya Kivule kwa tiketi ya Chadema amepokelewa rasmi na Wanachama pamoja na
Viongozi wa CCM jana katika kikao cha ndani.
Mbunge Viti maalum, Angelina Malembeko (kushoto) akizungumza na Viongozi na
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika Mkutano huo.Wapili kushoto ni Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam,
Cathe Kamba na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma.
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
wakisiliza kwa makini wakati wa Mkutano wa ndani wa Chama hicho wenye ajenda ya
kuwapokea rasmi Viongozi wa Vyama vya Upinzani ambao wamehami CCM.
Aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto (katikati) akipokelewa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi baada ya kuwasili katika Mkutano wa ndani wa Chama hicho wenye ajenda ya kuwapokea rasmi Viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani waliohamia katika Chama Cha Mapinduzi uliofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani wa Jimbo la Ukonga ambao
wamehamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
Baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani wa Jimbo la Segerea ambao
wamehamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Zingiziwa, Husein Togolo akizungumza na
Viongozi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mkutano wa
ndani wa Chama hicho wa kuwapokea rasmi viongozi pamoja na wanachama wa Vyama
vya upinzani ambao wanahamia CCM uliofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es
Salaam jana.
Aliyekuwa Diwani wa kata
ya Zingiziwa, Husein Togolo (kulia) akirudisha kadi ya Uwanachama wa Chadema
kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Cathe Kamba
wakati wa mkutano wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwapokea rasmi
viongozi pamoja na wanachama wa Vyama vya upinzani ambao wanahamia CCM
uliofanyika katika kata ya Pugu jijini jana. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo
la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akirudisha kadi ya Uwanachama wa Chadema kwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Cathe Kamba
wakati wa mkutano wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwapokea rasmi
viongozi pamoja na wanachama wa Vyama vya upinzani ambao wanahamia CCM
uliofanyika katika kata ya Pugu jijini jana. Katikati ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joyce Mkaugala.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akizungumza na
Viongozi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mkutano wa
ndani wa Chama hicho wa kuwapokea rasmi viongozi pamoja na wanachama wa Vyama
vya upinzani ambao wanahamia CCM uliofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es
Salaam jana.
Aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya
Vingunguti, Omary Kumbilamoto (kulia) akirudisha kadi ya Uwanachama wa CUF kwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Cathe Kamba
wakati wa mkutano wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwapokea rasmi
viongozi pamoja na wanachama wa Vyama vya upinzani ambao wanahamia CCM
uliofanyika katika kata ya Pugu jijini jana.Kushoto ni Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara.Kumbilamoto alikuwa ni Diwani Kata ya Vingunguti kwa tiketi ya CUF.
Aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala pia Diwani wa Kata ya
Vingunguti kwa tiketi ya CUF, Omary Kumbilamoto akizungumza na Viongozi pamoja
na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mkutano wa ndani wa Chama
hicho wa kuwapokea rasmi viongozi pamoja na wanachama wa Vyama vya upinzani
ambao wanahamia CCM uliofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Cathe Kamba akizungumza katika hafla
hiyo.
No comments