Breaking News

UONGOZI WA CCM MKOA WAZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MASHINA NA MATAWI UKONGA

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Chama kwa ngazi ya Wilaya, Joyce Mkaugala (wapili kulia) akizungumza na Wenyeviti na Kamati za Mashina, Viongozi wa Chama ngazi ya Tawi pamoja na Jumuiya ngazi ya tawi waliopo katika jimbo la Ukonga wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma akizungumza na Wenyeviti na Kamati za Mashina, Viongozi wa Chama ngazi ya Tawi pamoja na Jumuiya ngazi ya tawi waliopo katika jimbo la Ukonga wakati wa ufunguzi wa kikao cha ndani cha Chama hicho chenye ajenda ya kuandaa mikakati ya uchaguzi wa Ubunge na Udiwani kilichofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.

Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara akizungumza na  Wenyeviti na Kamati za Mashina, Viongozi wa Chama ngazi ya Tawi pamoja na Jumuiya ngazi ya tawi waliopo katika jimbo la Ukonga katika kikao hicho.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salamm, Saad Kusilawe akizungumza na Wenyeviti na Kamati za Mashina, Viongozi wa Chama ngazi ya Tawi pamoja na Jumuiya ngazi ya tawi waliopo katika jimbo la Ukonga wakati wa kikao cha ndani chenye maelekezo ya mikakati ya uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Ukonga pamoja na Udiwani kata ya Zingiziwa kilichofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.


Baadhi ya Wenyeviti na Kamati za Mashina, Viongozi wa Chama ngazi ya Tawi pamoja na Jumuiya ngazi ya tawi waliopo katika jimbo la Ukonga wakisililza kwa makini mada zinazoendelea katika kikao hicho kilichofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es Salaam jana.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe (mbele) pamoja na .Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara wakisalimia Wenyeviti na Kamati za Mashina, Viongozi wa Chama ngazi ya Tawi pamoja na Jumuiya ngazi ya tawi waliopo katika jimbo la Ukonga baada ya kumaliza kikao cha ndani cha chama hicho.

No comments