WAKAZI WA KATA YA KITUNDA,MZINGA,MSONGOLA NA KIVULE WAMPOKEA WAITARA KWA KISHINDO
Mgombea Ubunge Jimbo la
Ukonga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara (watano kushoto) akiongozana
na Viongozi wa
Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na
matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kuelekea katika Mkutano wa ndani wa Chama hicho wenye ajenda ya
kupata baraka kutoka kwa viongozi hao kwa fomu aliyochukua Waitara jijini Dar es Salaam jana kwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala pamoja na Kumtambulisha rasmi kuwa ni Mgombea Ubunge wa Jimbo
la Ukonga.Wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Ilala, Ubaya Chuma.
Katibu Mwenezi
wa CCM kata ya Kivule, Hemed Pogwa akizungumza na Viongozi wa
Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na
matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wakati wa Utambulisho wa Viongozi waliohudhuria katika mkutano
wa ndani uliofanyika katika kata ya Kivule jijini Dar es Salaam jana.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Wilaya ya Ilala, Fatuma Lomo akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya
Kivule, Hemed Nyunguru akizungumza na Viongozi wa
Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na
matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) waliopo katika kata ya Kitunda,Msongola,Mzinga na Kivule wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa ndani wa Chama hicho wa kumtambulisha mgombea Ubunge
Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara ulifanyika katika kata ya Kivule jijini Dar es
Salaam jana.
Mwanamuziki wa Muziki
wa Kizazi kipya (Bongo Fleva), Oscar Jeckonia (kulia) akitumbuiza katika mkutano huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya
ya Ilala pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Chama kwa ngazi ya Wilaya, Joyce
Mkaugala akizungumza na Viongozi
wa Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na matawi,Madiwani
na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
waliopo katika kata ya Kitunda,Msongola,Mzinga na Kivule wakati wa mkutano wa
ndani wa kumtambulisha rasmi Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara
uliofanyika katika kata ya kivule jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya
ya Ilala, Ubaya Chuma nae alizungumza katika hafla hiyo juu ya kumtambulisha
Waitara kuwa Mgombea wa Ubunge jimbo la Ukonga pamoja na kuwaomba Viongozi wa
Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na
matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kushirikiana na mgombea huyo katika Kampeni.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la
Ukonga, Mwita Waitara kwa Viongozi wa Halmashauri kuu ya kata na
matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali
za Mitaa waliotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopo katika kata ya Kitunda,Msongola,Mzinga na Kivule ambazo
zipo Jimbo la Ukonga wakati wa mkutano wa ndani uliochofanyika katika kata ya Kivule
jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi
ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara akizungumza na Viongozi
wa Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya Jumuiya ya kata na
matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) waliopo katika kata ya Kitunda,Msongola,Mzinga na Kivule wakati
wa kikao cha ndani cha kumtambulisha rasmi kuwa ni mgomboe wa jimbo la Ukonga
katika uchaguzi mdogo.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mianzini kwa tiketi ya Chadema , Gango Kidera ambaye amejIuzulu
na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) nae alizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya
Viongozi wa Halmashauri kuu ya kata na matawi, Mabaraza ya Jumuiya ya kata na
matawi, Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) waliopo katika kata za Kitunda,Msongola,Mzinga na Kivule wakisililza kwa makini wakati wa mkutano wa
ndani uliofanyika katika kata ya Kivule jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea Mbunge
wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kushoto) akisalimiana na Baadhi ya Viongozi
wa Halmashauri kuu ya kata na matawi, Mabaraza ya Jumuiya ya kata na matawi,
Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliotokana na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) baada ya kuwasili katika kikao cha ndani kilichofanyika jijini Dar es
Salaam jana kilichohusisha Viongozi hao katika kata ya Kitunda,Msongola,Mzinga na Kivule ambazo zipo katika Jimbo la Ukonga.
Mgombea Ubunge
Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri kuu ya kata na matawi,Mabaraza ya
Jumuiya ya kata na matawi,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa
waliotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumaliza kikao cha ndani
kilichofanyika katika kata ya Kivule jijini Dar es Salaam jana.
No comments