WAITARA AFANYA ZIARA KATIKA KAMPUNI YA MAGAZETI YA MWANANCHI COMMUNICATION LIMITED (MCL)
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akisalimiana na baadhi ya Wahariri wa Kampuni ya magazeti ya Mwananchi Communication Limited (MCL) jijini Dar es Salaam leo baada ya kuwasili ofisini kwao kwa ajili ya ziara yake ya kuzungumza na waandishi wa Kampuni hiyo.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akipata maelezo mafupi kutoka kwa mwandishi wa Mwananchi Communication Limited (MCL) katika Kampuni hiyo.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akizungumza na waandishi wa Kampuni ya Kampuni ya magazeti ya Mwananchi Communication Limited (MCL) jijini Dar es Salaam leo baada ya kuwasili ofisini kwao kwa ajili ya ziara yake ya kuzungumza na waandishi wa Kampuni hiyo.Waitara amezungumza na waandishi wa Gazeti la Mwananchi juu ya sababu zilizomfanya yeye kutoka upinzani kuhamia Chama Cha Mapinduzi ni kukosa uhuru wa kufanya kazi kwasababu alipokuwa Chadema uongozi ulikuwa unambana yeye kushirikiana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi hivyo imekuwa ni vigumu kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Jimbo la Ukonga kwasababu wananchi wamemchagua Waitara kwa ajili ya kutatua kero zao jimboni hivyo basi amehama ili kutafuta mahali ambapo itakuwa ni rahisi kwake kupata ushirikiano wa kiserikali kutatua kero za Ukonga.
No comments