MBUZI CUP YAKUSANYA VIJANA PAMOJA KATA YA GONGO LA MBOTO
Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas
Rukiko (kulia) akizungumza na wachezaji wa Timu ya Juve Fc na Mikongeni Fc
kabla ya Mchezo wa fainali ya Ligi ya Mbuzi Cup iliyochezwa katika Uwanja wa Kibiniko
jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti Dorcas ameandaa ligi hiyo kwa lengo la
kuweka vijana pamoja na pia ni miongoni kutimiza ahadi ambazo kama Mwenyekiti
wa Mtaa wa Guruka Kwalala aliziahidi kwa vijana juu ya kuinua michezo katika
kata.
Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko (kulia)
akipeana mikono na wachezaji wa Timu ya Juve Fc katika fainali hiyo.
Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko (kulia)
akipeana mikono na wachezaji wa Timu ya Mikongeni Fc katika fainali hiyo.
Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko (wapili kulia)
akiwa amekaa na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja
na wakazi wa kata ya Gongo la Mboto katika fainali ya Ligi ya Mbuzi Cup
iliyochezwa katika uwanja wa Kibiniko jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Timu ya Juve Fc, Salum Moshi
akiwatoka Wachezaji wa Timu ya Mikongeni Fc katika mchezo wa fainali ya Ligi ya
Mbuzi iliyodhaminiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata
ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko iliyochezwa
katika Uwanja wa Kibiniko jijini Dar es Salaam. Mikongeni Fc iliichapa Juve
Fc kwa Bao 2-0. Lengo kuu la Ligi hiyo ni kuwaunganisha Vijana kuwa kitu kimoja
pia ni Mwendelezo wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutekeleza
ahadi ambazo walizoahidi kwa wakazi wa kata ya Gongo la Mboto juu ya kusapoti
Michezo.
Mchezaji wa Timu ya Mikongeni Fc, James
Kuzwa (kulia) akichuana vikali na Mchezaji wa Timu ya Juve Fc,Abdallah
Ramadhani katika fainali ya Ligi ya Mbuzi Cup iliyodhaminiwa na Diwani Viti
Maalum Manispaa ya Iala pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Guruka
Kwalala, Dorcas Rukiko iliyochezwa katika Uwanja wa Kibiniko jijini Dar es
Salaam. Mikongeni Fc iliichapa Juve Fc kwa Bao 2-0.
Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko (kushoto)
akizungumza na wachezaji wa Timu ya Juve Fc na Mikongeni Fc baada ya Mchezo wa
fainali ya Ligi ya Mbuzi Cup iliyochezwa katika Uwanja wa Kibiniko jijini Dar
es Salaam. Mikongeni Fc iliichapa Juve Fc kwa Bao 2-0. Mwenyekiti Dorcas
alikabidhi Mbuzi na Mpira kwa Timu ya Mikongeni Fc na Mpira mmoja kwa Timu ya
Juve Fc.
Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko (aliyevaa
miwani) akikabidhi Mbuzi kwa Wachezaji wa Timu ya Mikongeni Fc baada ya kuibuka
mshindi wa Kwanza katika Ligi ya Mbuzi Cup iliyodhaminiwa na Diwani huyo na
kuchezwa katika Uwanja wa Kibiniko jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala,
Dorcas Rukiko (kushoto) akikabidhi mpira kwa Kapteni wa Timu ya Juve Fc baada
ya kuibuka mshindi wa pili katika Ligi ya Mbuzi Cup iliyodhaminiwa na Diwani
huyo na kuchezwa katika Uwanja wa Kibiniko jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Timu ya Mikongeni Fc wakishangilia
baada ya kukabidhiwa Mbuzi wao na Diwani Viti Maalum Manispaa ya Ilala Pia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas
Rukiko.
No comments