Tanga Cement yajenga wodi ya wazazi Hospitali ya Wilaya ya Handeni
Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya
Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kulia), akishikana mikono na
Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni,Upendo Magashi, katika hafla ambayo kampuni
hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi la hospitali ya wilaya hiyo pamoja na
samani zake lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Wengine ni
baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo. Hafla ya makabdhiano ilifanyika Handeni,
Tanga hivi karibuni.
Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya
Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Handeni, Mgaya Twaha (kulia), wakikata utepe kuashiria makabidhiano rasmi ya
jengo la wodi ya wazazi la hospitali ya
Wilaya ya Handeni lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87 na Tanga
Cement. Anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Upendo Magashi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha, akizungumza katika hafla ambayo Kampuni ya
Tanga Cement (TCPLC) ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi pamoja samani zake la
hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni mkoani Tanga. Kushoto ni Meneja
Kiwanda wa Tanga Cement, Mhandisi Ben Leman na kulia ni Katibu Tawala wa
Handeni, Upendo Magashi.
Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Helen Maleko
(kulia), akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi
ya wazazi pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada
kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni, Tanga
mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa wilaya na kutoka TCPLC.
Baadhi ya wananchi na wafahanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya
Handeni waliohudhuria hafla hiyo.
Viongozi wa kiserikali na
kisiasa pamoja na maofisa wa Tanga Cement wakipiga picha ya kumbukumbu mbele ya
jengo la wodi ya wazazi ya Hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa na
kampuni hiyo.
No comments