Airtel na itel wazindua SMARTPHONE mpya ya A32 F na Bando la Airtel BURE miezi sita
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu- kulia Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kati ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu baada ya kuzindua simu mpya ya A32 F ya smartphone kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel kwa pamoja wamezindua simu mpya ya itel A32 F iliyoambatanishwa na offer ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 12, dakika 300 pamoja na sms 300 kwa muda wa miezi 6 mfululizo.
Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A32F. Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuuu, Hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel.
Simu ya A32 F itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 12GB chenye muda wa miezi sita ambapo kila mwezi ni 2GB pamoja na nyongeza ya sms 300 na dakika 300 zote kutoka Airtel Tanzania.
Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam kutoka itel Mobile Mr. Walle XU, alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A32 F ambayo ni smartphone ya kwanza kutumia alama za vidole (finger print) yenye AndroidTM Oreo™ ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima. Simu ya A32 F ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu, alisema Khosla.
Bwana Walle aliongeza kuwa itel A32 F ina usalama na uhakika kwa kuwa inauwezo wa kutambua vidole vya mwenye simu na iweza kuweka programu nane ambazo zinatumika kwa matumizi mbalimbali kama kupiga picha, kupiga video, kupokea simu, stop alarm pamoja kusajili vidole vitano ambavyo kila kidole kinakuwa na kazi yake maalum.
Alisema vifaa vingine ni ukumbwa wake wa inch 5.0 pamoja na kamera ya kisasa ya 5mp kwa nyuma na mbele 2mp na inaweza kupiga picha kwa mazingira yeyote yale. Pia simu hiyo ina memory ya 8GB+1GB ambazo zinaweza kuzidi mpaka 32GB.
No comments