TBS WAWAFIKIA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO , TAMASHA LA BIASHARA LA WANAWAKE NA VIJANA AFRIKA
Na Adery Masta
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu ya alama ya ubora katika Tamasha la Biashara la Wanawake na Vijana Afrika (TABWA) lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Tamasha hilo leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam, Afisa udhibiti Ubora (TBS), Vaileth Kisanga amesema Wajasiriamali hao watakapopeleka bidhaa zao kupewa alama ya ubora, bidhaa hizo zitapimwa na maabara ambazo zimeidhinishwa na Shirika la Viwango Afrika (ARSO) ambapo majibu yao yatatumika katika nchi yeyote ya Afrika bila kikwazo.Aidha Vaileth amesema elimu waliyoitoa kwa wajasiriamali hao wadogo imepokelewa kwa muitikio mzuri ambapo wamewashauri kufika katika ofisi zao za kanda kwa ajili ya kupatiwa maelezo zaidi namna ya kusajili bidhaa zao ili kupata nembo ya ubora.Kwa upande wake, Mfanyabiashara kampuni ya PRM Products, Jane amelishuru Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kuwapatia elimu hiyo ambapo itamsaidia kuzisajili bidhaa zake ili ziwe na alama ya ubora ambayo itamsaidia kuaminika zaidi katika jamii.
MAONESHO hayo yamefanyika kwa awamu ya tatu na yameanza tangu Mei 28,2024,yatafika tamati June 2,2024 ambapo TBS imeitumia jukwaa hilo kwa ajili ya kujenga uwelewa kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kuhusiana na umuhimu wa alama ya ubora kwa lengo la kulinda afya za watumiaji wa bidhaa mbalimbali.
No comments