MUIGIZAJI GABO ALAMBA DILI NONO KIBOKO PAINTS
Mmoja wa Mafundi akiifanyia majaribio kwa kuipaka ubaoni bidhaa ya KIBOKO WALL PUTTY mbele ya mafundi wenzake ili kuwathibitishia ubora wake katika semina iliyofanyika Buguruni Jijini Dar Es Salaam ( kulia ni Bwn. Amani Nduli kutoka kampuni ya KIBOKO PAINTS na kushoto ni Bwn. Hamidu ambaye ni Afisa Mauzo )
Hayo yamebainishwa Leo , April 27, 2024 katika Semina iliyotolewa na Kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa Mafundi Rangi wa Buguruni na maeneo jirani.
Akizungumza baada ya Semina , Bwn. Hamidu ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema
Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam imeshafanyika Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu , Mbezi na hatimae Kariakoo .
" Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung'ara hata kama haujapigwa rangi " amesema Bw. Hamidu
"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni " amesema.
Aidha KIBOKO PAINTS imemtambulisha Muigizaji Gabo Zigamba kama Balozi wake, Muigizaji huyo ameahidi kufanya makubwa ili kuzitangaza bidhaa za KIBOKO.
.
No comments