KIBOKO WALL PUTTY YAWAFIKIA MAFUNDI MBAGALA
.
Baadhi ya Mafundi kutoka Mbagala , Chamazi na Maeneo Jirani Jijini Dar Es Salaam katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Utengenezaji , Uuzaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY kwa mafundi hawa , sambamba na hilo KIBOKO PAINTS imemtambulisha Muigizaji Salim Ahmed ( Gabo Zigamba ) kama Balozi wake, utambulisho uliofanywa na Afisa Masoko Mkuu wa Kampuni ya KIBOKO PAINTS Bwn. Erhard Mlyansi ( pichani ) Leo June 29 , 2024 katika Ukumbi wa DAR LIVE Mbagala Jijini Dar Es Salaam.
Mafundi wakiifanyia majaribio kwa kuipaka ubaoni bidhaa ya KIBOKO WALL PUTTY mbele ya mafundi wenzao ili kuwathibitishia ubora wake katika semina iliyofanyika DAR LIVE Jijini Dar Es Salaam.
Leo , June 29, 2024 akizungumza baada ya Semina , Bwn. Hamidu Satara ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema
" Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam zimeshafanyika Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu , Mbezi , Kariakoo , Mbagala na wiki ijayo tunatarajia kufanya Kigamboni "" Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung'ara hata kama haujapigwa rangi " amesema Bw. Hamidu
"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni " amesema.
No comments