TBS YAADHIMISHA SIKU YA VIWANGO AFRIKA NA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA INSHA.
Na Mwandishi Wetu.
Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) , Leo Machi 28, 2024 limeadhimisha siku ya viwango Afrika na kutoa vyeti na zawadi kwa Washindi 10 Bora wa Mashindano ya Insha ambapo Washindi wa nafasi tatu za Mwanzo ( waliopewa Zawadi za Fedha Taslimu) watashiriki Mashindano ya Insha Afrika.
Akizungumza katika Hafla iyo iliyofanyika makao makuu ya TBS Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hassan Bomboko ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Albert Chalamila , amelipongeza Shirika la Viwango Tanzania kwa kazi na Jitihada kubwa za kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na Bidhaa zilizo Bora hasa katika kipindi hiki cha Miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya SITA inayooongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
" Niwapongeze TBS kwa kuadhimisha siku hii muhimu kwa namna ya Kitofauti lakini pia niwapongeze washiriki wote zaidi ya 300 waliojitokeza kushiriki mashindano ya Insha hadi sasa tumewapata 10 bora , nyinyi kama wataalamu wetu wa badae wa masuala ya Viwango mmefanya jambo kubwa sana , Juzi wakati tukiadhimisha miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan TBS ni moja kati ya Mashirika yaliyofanya vizuri niwapongezeni sana " alisema Mhe. Bomboko
" Shirika la Viwango Afrika lilianzishwa mwaka 1977 likiwa na jukumu kuu la Kuoanisha viwango Afrika ili kukuza biashara na kupunguza vikwazo vya Kibiashara barani Afrika pamoja na kuimarisha ukuaji wa Viwanda Afrika .
No comments