NEEMA YA VUNA NA TIGO PESA YAWAFIKIA WAKULIMA, WAPEWA PIKIPIKI TV NA SIMU JANJA
Na Mwandishi Wetu.
Mtwara, Machi 5, 2024: Kampuni ya Tigo Tanzania leo imewazawadia wakulima walio katika mfumo ikolojia wa Tigo Kilimo kupitia promosheni iliyopewa jina la Vuna na Tigo Pesa katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani zawadi za kusisimua ikiwa ni kuonyesha shukrani kwa Kutumia Tigo Pesa kwa Msimu wa Mavuno uliomalizika 2022-2023.
Zuwena Ramadhan Semanda ( Kulia ) mkulima wa Korosho kutoka Lindi,akipokea zawadi ya Pikipiki kutoka kwa Kanali Patrick Sawala Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, ikiwa kama ZAWADI baada ya kuibuka mshindi wa PROMOSHENI YA VUNA NA TIGO PESA kwa wakulima KUTOKA MIKOA YA MTWARA, LINDI NA PWANI.
Kupitia huduma za Tigo Kilimo, Tigo Pesa na TCDC imeshirikiana kimkakati kufikia na kupanua huduma za kifedha za kidijitali kwa zaidi ya vyama vya ushirika vya wakulima 400 (Agricultural Marketing Cooperative Societies-AMCOS), biashara za kilimo na Shirika la Biashara la Zanzibar (ZTC) ambapo Tigo , kupitia huduma zake za kifedha za simu za mkononi, Tigo Pesa, inasaidia mipango ya wakulima na kuwezesha suluhu za malipo ya kidijitali.
Katika mpango wa Tigo Kilimo, wakulima wanapewa fursa ya kuchagua chaguo lao la malipo wanalopendelea yaani akaunti zao za benki au kupitia akaunti zao za Tigo Pesa, ambapo wengi walichagua kulipwa kupitia TIGO PESA kutokana na Urahisi na Usalama wake.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya Vuna na Tigo Pesa, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha, alisema kuwa Tigo imeamua kuwazawadia wakulima hao kupitia promosheni hii ili kutoa nafasi sawa kwa wakulima wote waliochagua Tigo Pesa kama chaguo lao la malipo, Hii ni ishara ya shukrani kwa kufanya miamala na Tigo Pesa kwa msimu uliopita wa mavuno ulioisha 2023.
Kupitia Vuna Pesa na Tigo Pesa zaidi ya wakulima ishirini walijishindia zawadi kabambe zilizojumuisha Televisheni, Friji, Simu Janja, Pikipiki (boda boda) na nyingine nyingi.
“Tunawashukuru sana wakulima wetu wa Tigo Kilimo kwa kuiamini Tigo Pesa na kuwa nasi katika kipindi chote cha msimu uliomalizika 2023 na ndiyo maana Tigo iliamua kuwazawadia kupitia promosheni ya Vuna na Tigo Pesa kwa msaada wenu mkubwa kwa wakati huu tuliopo,
pia tukisherehekea tuzo ya Mtandao wenye Kasi kutoka Ookla, ambapo tumetajwa kuwa Mtandao wa Simu wenye kasi zaidi nchini Tanzania. Tunatazamia msimu mwingine wa kusisimua na tija wa 2024-2025”, alisema Pesha.
Akitaja mafanikio ya Tigo Kilimo, Pesha alisema kuwa Tigo Pesa imetoa malipo ya wakulima ya TZS 100 bilioni kwa wakulima zaidi ya 50,000 Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Pesha, kuna AMCOS 300 ndani ya jukwaa la Tigo Kilimo ambalo lina wakulima 11,000. Hadi sasa, jumla ya fedha zilizotolewa kupitia Tigo Pesa katika mikoa mitatu ya Mtwara, Lindi na Pwani ni zaidi ya TZS bilioni 5.1 huku zaidi ya TZS 20 bilioni zimetolewa kwa wakulima nchini kote.
Pesha aliwahimiza wakulima na wateja wengine wa Tigo Pesa kuendelea kufanya miamala ya biashara zao kupitia Tigo Pesa kwa sababu ni njia rahisi, na salama zaidi ya kufanya miamala yao ya Kifedha kila siku kupitia simu ya mkononi.
No comments