TIGO WAWEZESHA USAJILI NA UTOAJI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO ZAIDI YA MILIONI 8 NCHINI , SASA ZAMU YA DAR ES SALAAM
Na Adery Masta.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa Watoto zaidi ya milioni 8.8 wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya miaka mitano.
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango leo Desemba 08, 2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huu unahitimisha Mikoa 26 ya Tanzania bara ambapo Mkoa wa Dar es Salaam unatarajiwa kusajili jumla ya watoto 248,298 na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo kupitia vituo 505 vya usajili ambavyo ni Vituo vya Afya na Ofisi za Watendaji wa Kata.
Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Mahusiano ya Nje Tigo Bi. Rukia Mtingwa amesema
"Tigo inayo furaha kwa mara nyingine tena kuendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania na wadau wengine wa maendeleo kwa kutekeleza mkakati huo wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa 26 sasa Tanzania nzima
Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini Tanzania. Tunajivunia mafanikio ya sekta hii.
No comments