Breaking News

DIT WATOA TUZO NA ZAWADI ZA FEDHA KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI 2022 / 2023

 



                               

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msofe ( aliyevaa tai ) katika moja ya banda la bunifu mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi wa DIT , muda mchache kabla ya kuingia ukumbini kutunuku Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri 2022 / 2023

Na Mwandishi Wetu.

Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam DIT Leo , Desemba 6 , 2023 imefanya hafla ya kuwatambua na kuwatunuku vyeti na zawadi za Fedha hadi Milioni Moja na laki tatu wanafunzi waliofanya vizuri katika mwaka wa Masomo 2022 / 2023 , Tukio lililohudhuriwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msofe ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia .

Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti hivyo Prof. Msofe ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam , kwa kuona umuhimu wa kufanya jambo hili maana linatia hamasa kwa wanafunzi waweze kusoma kwa bidii na kuwa wabunifu zaidi
" Nilipongeze baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam kwa kuona umuhimu wa kuwatunuku vyeti na kuwapa zawadi wanafunzi wanaofanya vizuri lakini pia niwapongeze wafadhili wanaowezesha tukio hili kwa maana linawafanya wanafunzi waipende fani ya Uhandisi na kuchochea ukuaji wa fani hii nchini , Nahimiza Taasisi kuendelea kuandaa na kuboresha tukio hili na Wizara itakua ikiwaunga mkono muda wote " Alisema Prof. Msofe
Naye kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam Prof. Preksedis Ndomba amesema Taasisi inaandaa Tuzo hizi ili kujenga ushindani na kuhamasisha juhudi katika masomo baina ya wanafunzi , Tumekua tukitoa Tuzo hizi kwa zaidi ya miaka 20 sasa na huwa Tunaziboresha kila mwaka " amesema Prof. Ndomba

Mwisho

No comments