TAASISI YA MY LEGACY NA HABITAT FOR HUMANITY TANZANIA NEEMA MASHULENI , DC KINONDONI AFUNGUKA
Taasisi isiyo ya kiserikali (My Legacy) kwa kushirikiana na Taasisi ya Habitat for humanity Tanzania (HFHT) wamekabidhi matundu ya vyoo 20 katika shule za sekondari 4 na shule ya msingi 1 lengo ikiwa ni kuboresha maeneo ya kujifunzia na kusaidia watoto wa kike wakiwa katika hedhi.
Shule hizo zilizofikiwa ni Shule ya Sekondari Daniel Chongolo, Kisauke, Maendeleo, Twiga Sekondari na shule ya msingi Mtakuja.Akizungumza wakati wa makabidhiano ya matundu hayo ya vyoo katika shule ya Sekondari Daniel Chongolo iliyopo mbezi Beach B, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule alisema serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi ya My Legacy kuhakikisha ujenzi wa vyoo mashuleni unafanyika kwa viwango vya juu.
Mtambule aliwasisitiza wanafunzi wa shule hizo ambao wamekabidhiwa vyoo hivyo kuhakikisha wanatumia vizuri vyoo hivyo kwa kuzingatia usafi ili vije kutumika na vizizi vijavyo.
Aidha alisema Sekta ya Elimu katika Wilaya ya Kinondoni, serikali imetuletea zaidi ya shilingi Bilioni 12 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya elimu ambapo hadi sasa shule nyingi zinajengwa lakini pia kuondoa ada mashuleni
"Hizi ni jitihada zinazofanywa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha adui ujinga anaendelea kutokomezwa"Kwenye eneo la uchumi Mtambule alisema nchi yetu imeendelea kufanya vizuri ambapo mwaka 2020 Tanzania ilitajwa na Benki ya Dunia kwamba ni nchi iliyoingia kwenye uchumi wa kati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali, My Legacy Fortunata Temu aliiomba jamii kuona umuhimu wa kushiriki katika kuhakikisha wanaweka miundombinu rafiki na upatikanaji wa lishe kwa watoto mashuleni lakini pia ulinzi wa watoto ili kuepusha vitendo vya ukatili na unyanyasaji ili watoto wawe katika mazingira salama.
Mbali na hayo Temu alisema mwaka 2024 Taasisi yao imepanga kuanzisha programu ya Kuhamasisha jamii kuchangia maendeleo kama wanavyochangia shughuli mbalimbali za kijamii ambapo wanatarajia kuchangisha fedha na vifaa ili waweze kujenga vyoo zaidi kwani uhitaji bado ni mkubwa"vyoo tunavyovikabidhi ni sehemu ya mradi wa WASH ambapo mbali na kukabidhi vyoo hivi mashuleni, pia tunarajia kujenga vyoo vingine kwa wingi zaidi katika shule nyingine zenye uhitaji".
"Tutaiomba serikali yetu sikivu kutuunga mkono kwenye suala hili ili tuweze kufanikisha jambo hili" Alisema
Naye mratibu wa Program na utafutaji rasilimali wa Taasisi ya My Legacy, Amina Ally alisema utoaji huo wa vyoo mashuleni ni sehemu ya kuboresha maeneo ya kujifunzia na kusaidia watoto wa kike wakiwa katika hedhi.Aidha alisema Shirika la My Legacy kwa kushirikiana na Taasisi ya Habitat wameendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wote hasa wa kike wanaishi kwenye mazingira yenye staha na yenye kulinda utu wao kutokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Tumefanya hivi kupitia programu zetu mbalimbali ambazo zimejikita katika kutengeneza mifumo ya upatakinaji huduma za WASH ikiwemo maji safi na kusaidia watoto wa kike waliokwisha kubalehe kuweza kujisitiri na kuwa wasafi wakati wa hedhi"
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa ya Mbez beach B, Asha Voniatis alisema wamekuwa na ushirikiano wa karibu na Tasisi hiyo ya My Legacy katika maeneo mbalimbali ambapo shirika hilo walikuwa mstari wa mbele wakati wa UVIKO-19 ambapo walihakikisha wanapata elimu ya usafi ikiwemo unawaji wa mikono, utengenezaji wa sabuni na kuwapatia vifaa mbalimbali vya kujikinga na Janga hilo.
Mwenyekiti huyo aliwapongeza kwa kuwapa kipaumbele wanawake na vijana kwa kuwapa semina ili kuhakikisha wanaongeza elimu katika kuongeza nguvu kwenye ujasiliamali ambapo hadi sasa wapo vijana ambao wamejiajiri hasa katika utengenezaji wa sabuni.
"Tulijifunza kutengeneza mkaa kwa kutumia nataka ya makox, suala la mazingira ni kipaumbele sana na hivyo tuliwapatia wakina mama wasiopungua 200 elimu ya utengenezaji mkaa ili kuweza kupunguza taka zikizokuwa zikizagaa mtaani na zimeounguza gharama za kununua mkaa na imepelekea kuongeza ajira kwa watu wengine"
Kadhilika Voniatis alimshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwekeza katika suala la elimu ambapo hadi sasa wanafunzi wanapomaliza shule za msingi wote wanakwenda sekondari.
Mwakilishi kutoka Habitat for humanity Tanzania (HFHT), Flavian Ngeni alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali na wadau kutoa huduma kwa jamii ambayo Ina uhitaji mkubwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa shule ya Sekondari ya Daniel Chongolo, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Selvia Lyimo alisema Mradi huo utasaidia kupunguza utoro mashuleni lakini pia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu
No comments