MY LEGACY WAHITIMISHA SEMINA YA SIKU TATU NA WADAU HAWA MUHIMU
Wadau katika Sekta zote wametakiwa kuhakikisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wanashirikishwa katika maamuzi yanayohusiana na umiliki ardhi, kujua sheria zinazohusiana na ardhi na wapi wataweza kwenda kupata haki zao pale zinapokuwa wzimedhurumiwa.
Hayo yalisemwa juzi na Mratibu kutoka Taasisi ya MyLEGACY Amina Ally wakati wakifunga warsha ya siku tatu ya wadau kuhusiana na masuala ya ardhi kwa wanawake, vijana na watu wanaoishi na UlemavuWadau hao ni wawakilishi kutoka Taasisi za kidini, viongozi wa Kata mbalimbali, maafisa maendeleo, maafisa ustawi lakini pia wadau kutoka Mashirika ambao wanafanya kazi katika jamii kwa ngazi za Taifa lakini pia Mashirika ya ayofanya kazi kwa ngazi ya chini katika jamii
"Kwa siku hizi tatu tumeweza kuchambua au kujifunza kuhusiana na sheria mbalimbali kuhusiana na masuala ya ardhi kwa wanawake, vijana na watu wanaoishi na Ulemavu pia kuangalia ni jinsi gani kwa pamoja tunaweza kufanya uchechemuzi wa masuala au changamoto zinazohusiana na masuala ya umiliki upatikanaji wa ardhi katika makundi hayo katika ngazi ya chini"
"MyLEGACY imefanya utafiti ambao ulikwenda kuangalia changamoto zilizopo Katika upatikanaji wa ardhi au kumiliki ardhi kwa wanawake, vijana na watu wanaoishi na ulemavu ambapo tumekuta bado kuna changamoto mbalimbali hasa zinazotokana na Mila na sheria nyingine kushindwa kujumuisha makundi kama watu wanaoishi na Ulemavu na sheria zinazozuia wanawake kumiliki ardhi au Mali ambazo hazihamishiki kama nyumba hasa katika mirathi"Alisema zipo sera ambazo hazikidhi mlengwa wa kijinsia na kuhusisha watu wanaoishi na Ulemavu kuhakikisha na wao wanapata makazi yenye staha ikiwa ni pamoja na kumiliki ardhi ili waweze kuwa na makazi rafiki na kujiendeleza kiuchumi.
Akifafanua kuhusu takwimu za ushriki wa watu wenye ulemavu katika mijadala ya upatikanaji ardhi, Mratibu huyo alisema asilimia 10.1 watu wenye ulemavu wanashiriki katika michakato ya majadiliano kuhusiana na ardhi lakini pia asilimia 43.6 hawajui kama kuna miundombinu yoyote iliyopo ya upatikanaji wa haki ya umiliki ardhi.
Kwa upande wake Katibu kutoka Wilaya ya Kinondoni katika kampeni huru ya shujaa wa Maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA), Fatma Hamisi alisema kumekuwa na sheria kandamizi ambazo huwa zinamkandamiza mwanamke ambazo zinawanyima baadhi ya vijana na watu wenye ulemavu katika umiliki ardhi ambapo dhana hizo zinaweza kuondolewa kutokana na elimu waliyoipata katika warsha hiyo.
"Ili jamii iweze kutambua haki zao lazima tuweze kushuka katika ngazi za chini ambapo jamii inapatikana kwa kuweza kuwapa elimu ili iweze kuwapa uelewa kwamba umiliki wa ardhi ni haki ya Kila mmoja"
Naye katibu wa SMAUJATA katika Wilaya ya Ubungo Grantmond Sentala aliwapongeza MyLEGACY kwa kushirikisha wadau kwaajili ya warsha hiyo ya siku 3 ili kutoa elimu kuhusu Habari ya umiliki kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
"Tumegundua kwamba kuna sheria zinazowakandamiza lakini kuna taratibu za kimila ambazo zimekua changamoto katika jamii zetu ambazo zinawakandamiza wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa upande wa kumiliki ardhi, zipo familia inayomilikisha mtu ardhi lakini hawana nyaraka ambazo zitamfanya mmiliki ardhi atambulike kisheria au kiserikali, hivyo sisi kama wadau tutaenda kwenye ngazi za kijamii familia pamoja na watu wenye makundi maalumu kuzungumza nao kwamba pale wanapogawa urithi wajaribu kuweka kwa njia ya dokimenti ili katika umiliki ardhi serikali iweze kuwatambua"
No comments