TIGO YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2023 MKOANI IRINGA
Na Mwandishi Wetu.
Mtandao namba moja kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali nchini Tigo , umezindua wiki ya Huduma kwa wateja Mkoani Iringa ikiwa na Kauli mbiu ya TEAM SERVICE akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Wiki hii ya Huduma kwa wateja kote duniani ambayo huwa ni Wiki ya kwanza ya Mwezi Oktoba Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tigo Bi. Mwangaza Matotola amewapongeza wafanyakazi na wateja wa Tigo kwa kuendelea kuwaamini
" Napenda kuwashukuruni nyote kwa kuungana nasi katika siku hii adhimu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja na leo ikiwa ni ufunguzi rasmi wa maadhimisho haya ,Tigo inafuraha kuungana na watoa huduma ulimwenguni kote kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Octoba kila mwaka na kwa mwaka huu itaadhimishwa kuanzia tar 2– 9 Octoba.
Tigo inatambua kazi kubwa inayofanywa na team ya wataalam wetu wa huduma kwa wateja zaidi ya 1000, wanaohudumia wateja zaidi ya milioni 13 nchi nzima. Kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu “Team Service ”, inaonesha umuhimu wa watoa huduma wetu kufanya kazi kwa pamoja ili kutoa huduma bora kwa ufanisi kwa wateja wetu wote.
Kupitia wiki hii ya huduma kwa wateja, Tigo inadhamiria kukuza uelewa wa wateja wetu juu ya taaluma ya huduma kwa wateja na wakati huo huo ikitambua na kuwashukuru wataalamu wetu wote waliopo mstari wa mbele kutoa huduma zenye ubora kwa wateja wakati wote.
Tigo ni mtandao wa watu unaoongoza kwa ubunifu unaozingatia mahitaji ya wateja. Ubunifu huu unadhihirika katika namna tunavyohudumia wateja wetu kupitia njia mbalimbali kama; namba 100 – kuongea na muhudumu kwa wateja, namba 100 kujihudumia kwa njia ya sauti, mitandao ya kijamii na katika maduka yetu zaidi ya 52 nchi nzima.
Umahiri wa watoa huduma wetu pamoja na ubora wa huduma za Tigo umepelekea wateja wetu kuendelea kupendekeza huduma zetu kwa ndugu,jamaa na marafiki kwa kiwango cha juu cha asilimia 80. Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuendelea kutuamini " amesema Bi. Matotola
No comments