Breaking News

TIGO YAWEZESHA KONGAMANO LA MADINI NA UWEKEZAJI 2023

 Na Mwandishi Wetu.

Kampuni Namba moja nchini kwa utoaji wa huduma za kidigitali Tigo Tanzania imewezesha na kutoa Huduma katika Kongamano la Madini na Uwekezaji Tanzania (  Tanzania Mining and Investment Forum 2023 ) linaloendelea katika Ukumbii wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ( JNICC)  Jijini Dar Es Salaam , Kampuni hii imewezesha Kongamano hili kwa namna kuu mbili Mosi,  Kwa kutoa Intaneti ya BURE na yenye Kasi ( FREE WI-FI ) kwa washiriki wote wa Kongamano hili kutoka ndani na nje ya nchi , na Pili kama watoa Huduma za mawasiliano kwa Makampuni na mashirika mengi ambayo yapo katika sekta hii ya Madini. 

Akizungumza Jana Oktoba 25, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Huduma na TEHAMA Tigo Business Bwn. Norman Kiondo amesema 


" Tigo kupitia masuluhisho yake mengi inaunga mkono Agenda ya Kitaifa ya kuiweka nchi katika Dunia ya Kidigitali na Sisi kama Kampuni tunayo masuluhisho ambayo yanasaidia makampuni yanayojishugulisha na Madini kuweka kufanya shughuli zao katika namna ya Kiteknolojia zaidi kuongeza Ufanisi,  Kupunguza gharama na kuongeza usalama wa wafanyakazi wao "

Aidha Bwn.  Kiondo ameongezea kuwa  Tigo inayo masuluhisho kama Internet of Things ( Iot ) ambazo zimewezesha makampuni na mashirika mengi kuweza kufanya huduma zao kwa namna ya Kiteknolojia Huduma kama Ku TRACK Magari na Vifaa vingine kuweza kujua vilipo na usalama Wake kiujumla,  Huduma nyingine ni Kidigal Enabled Workforce ambapo mfanyakazi anapoingia Mfano mgodini anakua ameunganishwa na Msimamizi Wake anaweza kuona chochote kinachoendelea hii inaongeza ufanisi na Usalama wa Wafanyakazi. 
Aidha Tigo wamewakaribisha washiriki wote wa Kongamano hili katika banda lao ili kujionea na kupata Ufafanuzi wa Mambo mengi mazuri waliyonayo.

No comments