Breaking News

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 



Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo ilikuwa na kaulimbiu ya "TEAM SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki yake kuendelea kutoahuduma bora kwa wateja wake.

Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati) akikata keki pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja katika tawi la Mlimani City jijini Da es Salaam. hivi karibuni ambapo ilikuwa na kaulimbiu ya "TEAM SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki yake kuendelea kutoahuduma bora kwa wateja wake.



Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki hiyo


Baadhi ya maofisa wa Tanzania Commercial Bank pamoja na wateja wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.

 

Tanzania Commercial Bank jana iliungana na mataifa mbalimbali duniani kote kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa mteja kwa mwaka 2023 ilikuwa na kaulimbiu ya “TEAM SERVICE” hiyo huku benki hiyo ikijikita zaidi na dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora na  zinazokidhi mahitaji ya wateja.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki wa huduma kwa wateja Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa benki hiyo ambaye ni mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya alisema benki ya TCB inachukulia kwa ukubwa wa hali ya juu sana kutoa  huduma kwa wateja ndiyo maana kwa Tanzania commercial bank huduma ni moja ya mikakati na utamaduni wa benki hiyo.

 

Msuya alisema “kaulimbiu ya mwaka huu  inaendana hasa na utekelezaji wa majukumu yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu wa Tanzania Commercial Bank na kuboresha huduma ni hamasa ya biashara na TCB imeweka kipaumbele cha kutoa huduma bora kwa wateja”.

 

"Hii ndiyo sababu Tanzania Commercial Bank inaendelea kuwekeza mara kwa mara katika jamii na kuwapa wafanyakazi wetu ujuzi na rasilimali zinazohitajika ilikuhakikisha wanawapa wateja wetu huduma za hali ya juu," Msuya alisema.

No comments