TBS YARAHISISHA ZOEZI LA UKAGUZI WA MAGARI NJE YA NCHI , WASAINI MKATABA AN KAMPUNI ZA QISJ NA EAA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) Dkt. Yusuph Ngenya (kushoto) baada ya kusaini mkataba na Bw. Brian Kuria ( kulia ) Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ukaguzi wa magari ya Quality Inspection Services Japan ( QISJ) ambayo imeshinda zabuni ya kukagua magari yanayotoka nchi za Falme za Kiarabu (UAE) yatakayoletwa hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) Dkt. Yusuph Ngenya (kushoto) baada ya kusaini mkataba na Bw. Toyohiko Hashino ( kulia ) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa EAA Company Limited kampuni ambayo imeshinda zabuni ya kuisaidia TBS kufanya ukaguzi wa magari katika nchi ya Uingereza yanayotarajiwa kuletwa hapa nchini.
WAWEZA KUTAZAMA VIDEO HAPA
Na Mwandishi Wetu.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Leo , June , 26. 2023 limesaini Mikataba na Kampuni za EAA na QISJ kwaajili ya kufanya ukaguzi wa magari katika nchi ambazo kampuni hizo zimeshinda zabuni , katika kuhakikisha magari yanayoingizwa nchini yanakuwa na ubora.
Akizungumza Mkurugenzi mkuu wa TBS Dkt Yusuph Ngenya amesema wameingia makubaliano na kampuni za EAA na QISJ ili kusaidiana kuwa na magari yenye ubora nchini.
Moja wapo ya majukumu ya TBS ni kufanya ukaguzi wa magari yaliyotumika yenye Zaidi ya miaka mitatu tangu kutengenezwa (used Moto vihcles) yanayotoka nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa yanakidhi vigezo vya ubora na usalama kabla ya kuingia nchini. Kwa mjibu wa utaratibu magari hayo ukaguliwa kwenye nchi yanakotoka kabla ya kuletwa hapa nchini kwa utaratibu uitwao ( Pre shipment Verification of Conformity to Standard (PVoC). Ukaguzi wa magari kabla ya kuletwa nchini ufanywa na mawakala wa ukaguzi wanaofanya kazi iyo kwa niaba ya TBS ambapo yale yanayokidhi matakwa ya viwango upewa cheti (Certificate of Roadworthiness). Magari yaliyokaguliwa nje ya nchi yanapofika nchini ufanyiwa ukaguzi wa uhakiki (verification Inspection ) ili kudhibitisha yanakidhi vigezo vya kiwango vya kitaifa (TZS 698:2012).
Mawakala wanaofanya ukaguzi wa magari pamoja bidhaa nyingine upatikana kwa utaratibu wa zabuni ivyo wale wanaoshinda vigezo vya zabuni uingia Mkataba na TBS. Mawakala wa Ukaguzi ufanya kazi katika nchi yanakotoka magari mengi yanayoletwa hapa nchini ambazo ni pamoja na Japani, Uingereza, Falme za Kiarabu (UAE) kuanzia mwezi julai 2022 Ukaguzi wa magari katika nchi ya Japani umekuwa ukifanywa na kampuni iitwayo (EAA Co Ltd ) ambayo ilishinda zabuni ya ukaguzi wa magari kutoka nchi iyo yanayotarajiwa kuletwa nchini Tanzania.
Hivi karibuni kampuni ya EAA pia imeshinda zabuni ya kufanya ukaguzi wa magari katika nchi ya Uingereza yanayotarajiwa kuletwa hapa nchini. Vilevile, hivi karibuni kampuni iitwayo Quality inspection services Japan ( QISJ) imeshinda zabuni ya kukagua magari yanayotoka nchi za Falme za kiarabu (UAE) yatakayoletwa hapa nchini. TBS imesaini mikataba na kampuni za EAA na QISJ kwaajili ya kufanya ukaguzi wa magari katika nchi ambazo kampuni hizo zimeshinda zabuni. Idadi ya magari yaliyotumika yanayokaguliwa kwa mwaka yanakadiliwa kuwa 46000 na Kati ya hayo 92% yanatoka Japan 4% yanatoka uingereza 1% yanatoka nchi za farume za kiarabu na kiasi kilichobaki utoka nchi nyinginezo.
Gharama za Ukaguzi nje ya nchi USD 150 kwa gari moja ( Sawa na wastani TZS 350,000 kwa gari) kurahisisha uondoshaji wa magari katika bandari ivyo kuongeza ufanisi wake kwani magari yaliyokaguliwa nje ya nchi yanapofika bandarini uondolewa kwa haraka. Kuwaondolea waingizaji itaji la kupeleka gari kwenye kituo cha ukaguzi baada ya magari kufika nchini, Kuepusha nchi kuwa jalala la magari yasiyokidhi viwango kwa kuyazuia Yale yasiyokidhi vigezo katika nchi yanakotoka kabla yakuletwa hapa nchini lakini pia utaratibu huu utasaidia Kuepusha gharama za kuharibu au kurudisha gari nchi ilikotoka pale endapo ikatokea kuwa baada ya kufika nchini ilibainika kuwa na kasoro kubwa zenye athari kwa afya na mazingira, Kuepusha gharama za matengenezo kwa mnunuzi kwani gari linapopimwa kabla ya kuwasili nchini kasoro zozote zinazobainika ushughurikiwa hukohuko kabla ya kuletwa nchini". Alimalizia Dkt. Ngenya
Aidha Dkt. Ngenya ametoa Wito kwa wananchi wanaoagiza magari yaliyotumika kutoka nje ya nchi kuzingatia utaratibu wa kuhakikisha kuwa magari hayo yanakaguliwa kabla ya kuletwa nchini na kupata cheti cha kudhibitisha kukidhi matakwa ya viwango (certificate of Roadworthiness).
No comments