Breaking News

TBS WATOA ELIMU YA UMUHIMU WA VIWANGO KWA WAJASIRIAMALI , MAADHIMISHO YA WIKI YA BARCODE 2023.

 



Afisa Masoko TBS Bi. Rhoda Mayugu ( kulia ) akiwaelezea baadhi ya wajasiriamali ( katika nyakati tofauti tofauti ) umuhimu wa Viwango na namna ambavyo serikali imeweza kuhakikisha inawapa unafuu wa gharama ambazo zinahusika katika ufikishaji ubora, katika Maadhimisho ya Wiki ya BarCode Kitaifa 2023 yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam.



Afisa Udhibiti Ubora TBS Bi. Beatrice Lena ( kushoto ) akiwaelezea baadhi ya wajasiriamali ( katika nyakati tofauti tofauti ) umuhimu wa Viwango na namna ambavyo serikali imeweza kuhakikisha inawapa unafuu wa gharama ambazo zinahusika katika ufikishaji ubora, katika Maadhimisho ya Wiki ya BarCode Kitaifa 2023 yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam.

Na Mwandishi WETU.

 Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) limeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya BarCode Kitaifa 2023 yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam ambapo TBS kama wadau kutoka Sekta ya Viwanda na Biashara wamealikwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali ambazo zinahusiana na namna bora ya kuzalisha bidhaa hili ziweze kufikia matakwa ya Viwango. 

TBS wametembelea wajasiriamali mbalimbali walioko katika maadhimisho hayo na kuwaelezea namna bora ya kuweza kuthibitisha bidhaa zao ili waweze kupata alama ya Ubora katika bidhaa zao na umuhimu wake katika kupenya masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Akizungumza katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya BARCODE kwa mwaka 2023, Afisa Udhibiti Ubora kutoka TBS Bi. Beatrice Lena amesema kuwa 

" Kupitia Maadhimisho haya , tumewaelezea Wajasiriamali namna ambavyo serikali imeweza kuhakikisha inawapa unafuu wa gharama ambazo zinahusika katika ufikishaji ubora wa bidhaa ambapo kwa sasa wajasiriamali watahitaji kuwa na barua ya Utambulisho kutoka SIDO , na hapo wataweza kujisajili katika mfumo wa Kielektroniki wa TBS ambapo baada ya hapo TBS tutamhudumia bure kwa muda wa miaka mitatu bila kuwa na gharama yoyote mpaka mwaka wa nne atakapoanza kuchangia 25% ambayo hiyo itaendelea kuongezeka kwa kila mwaka mpaka atakapofikisha asilimia 100 , TBS imeendelea kuwakumbusha wajasiriamali kuwa hii ni fursa muhimu sana kwao kwasababu itawasaidia katika kuhakikisha wanapata unafuu wa gharama za kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na kupenya katika masoko ya ndani na nje ya nchi".

Pia TBS imeyatumia Maadhimisho haya yaWiki ya  BARCODE 2023 kutoa elimu kwa wananchi wa kawaida waliotembelea banda lao kuhusu umuhimu wa kuangalia muda wa matumizi ya bidhaa wanaozinunua lakini pia kuangalia alama ya ubora katika bidhaa wanazozinunua ili kuhakikisha wanatumia bidhaa ambazo ni bora kwa afya zao.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HAPA


No comments