TCCIA KUANDAA MAONESHO MAKUBWA MLIMANI CITY DAR
Rais wa Chemba ya Biashara Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Paul Koyi (kushoto) akizungumza wakati wa kutangaza Maonesho ya Biashara pamoja na ziara za kibiashara kwenda nchi za China na Ujerumani Hatua hiyo inaendana sambamba na utekelezaji wa majukumu ya chemba ambapo maonesho hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam eneo la Viwanja vya Mlimani City kati ya Oktoba 10 hadi 14, 2019. hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za TCCIA Dar es Salaam hivi karibuni mwengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Gotfrid Muganda.
CHEMBA YA BIASHARA ,VIWANDA NA KILIMO TANZANIA
TAARIFA KWA WAFANYABIASHARA
Ndugu wanahabari,
Habari ya asubuhi.
Dar es Salaam, Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania imetangaza kuandaa
Maonesho ya Biashara pamoja na ziara za kibiashara kwenda nchi za China na Ujerumani.
Hatua hiyo inaendana sambamba na utekelezaji wa majukumu ya chemba ambapo maonesho hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam eneo la Viwanja vya Mlimani City kati ya Oktoba 10 hadi 14, 2019.
“Tutakuwa na makampuni ya hapa nchini ambayo yataonesha bidhaa zinazolishwa na viwanda vyetu nchini,pia kutakuwepo na taasisi ambazo zinatoa huduma mbalimbali kwa wafanyabiashara na jamii kwa ujumla. Tunawajulisha wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuja ili kunufaika na bidhaa na huduma hizo,”ilfafanua taarifa hiyo Rais wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania Paul Koyi.
Kwa mujibu wa chemba hiyo, faida zake ni kwa mtumiaji wa bidhaa husika kukutana moja kwa moja na mzalishaji ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu bidhaa na huduma husika.
Pia kwa wazalishaji inawasaidia kubani bidhaa na teknologia mpya ili kujifunza zaidi na kuboresha za kwao ili kumudu ushindani alisema koyi.
Aliongeza kwakusema kuwa aidha, kwa wafanyabiashara yanawasaidia kuona fursa zilizopo na kupanua wigo wa mtandao wa kibiashara.
Wakati huo huo, Chemba hiyo imeeleza kuwa watakuwa na ziara ya kibiashara kwenda China na Ujerumani.
Ziara hii itakuwa ni ya siku kumi kuanzia Oktoba 24,2019 hadi Novemba 5, mwaka huu.
“Wafanyabiashara wa Tanzania watatembelea viwanda vya China kwenye miji ya Quandzhou,Foshan na Shenzen. Miji hii ni maalum kwa mashine,utaalam wa samani, vifaa vya umeme,nguo,taa na vifaa vyake,viatu na mabegi.
“Bidhaa hizi zinatumika katika matumizi ya kila siku,hivyo ni ziara ya kuongeza utaalam na kupanua wigo wa mtandao wa kibiashara,”ilifafanua.
Katika ziara ya Ujerumani itakuwa ni ya siku tano kwenye mji wa Berlin,Ujerumani kuanzia Novemba 5-10, 2019. Ziara hii italenga zaidi kutafuta masoko katika sekta za utalii,matunda,viungo na kahawa. Sambamba na masoko pia italenga kutafuta mashine za kusindika mazao yetu.
“Tukichukua ziara ya karibuni ambako tulikuwa na makampuni 52 ambayo ilifanyika mwezi wa nne mwaka huu nchini China na hata za kwaka jana 2018 ni kwamba washiriki baada ya ziara walioshiriki ziara hiyo wameweza kunufaika kama ifuatavyo.
Wengi wao wameomgeza wigo wa biashara zao,mfano aliyekuwa anafanya biashara tu ya hoteli ameweza kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mifuko hii mbadala ya kubebea. Na sasa ni muuzaji mkubwa kanda ya kati.
Pia wenye mashine za kusaga nafaka,wameweza kuwa na mashine za kukausha mazao mapema mfano mahindi na mpunga badala ya kutegemea jua.
Pia kuna mwingine ambaye anamiliki hospitali ameweza pia kuanzia kiwanda cha kutengeneza maji,na hii ni baada ya kupata mitambo ya mnyororo mzima wa uzalishaji wa maji ya chupa. Hizo zikiwa na mifano,kwani wengi wamepanua wigo wa biashara zao.
No comments