Benki ya DCB yadhamini Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania
Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jaffo, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Godfrey Mweli.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa, Joseph Kandege (kulia), akishiakana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa baara ya kupokea cheti cha shukurani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, kutoka na udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akimfahamisha Angel Lomwai kuhusu faida ya akaunti maalumu ya mpango wa elimu ya ‘DCB Skonga’ iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Ofisa Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Dalila Issa (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu akaunti maalumu ya masuala ya elimu ya DCB Skonga iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini.
Baadhi ya wahudhuriaji katika hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini wakifuatilia matukio mbalimbali ya utoaji tuzo hizo.
BENKI ya Biashara ya DCB itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo ya elimu nchini huku ikileta bidhaa na huduma maalumu za kielimu zinazolenga kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora kwa mustakabali wa maendeleo yao binafsi na kwa taifa.
Akizungumza katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambazo DCB ilidhamini, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema DCB inatambua juhudi kubwa inayofanywa na Rais John Joseph Pombe Magufuli katika kuboresha na kuinua kiwango cha elimu nchini, juhudi zilizoanza kujionyesha mwanzo kabisa pale alipoondoa ada za shule kuanzia elimu ya msingi hadi Sekondari.
“Kwa kutambua umuhimu wa elimu Benki ya DCB hivi karibuni tulizindua akaunti maalumu iitwayo ‘DCB Skonga’ ikilenga kumsaidia mteja wetu kuweka akiba kidogo kidogo huku tukimpa uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufikia chuo kikuu.
“Kumekuwa na changamoto kubwa sana katika jamii inayotuzunguka pindi mzazi/mlezi anaetegemewa na familia anapopoteza maisha au kupatwa na ulemavu wa kudumu, kwani watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo hii imetengeneza hofu kwenye familia nyingi. Kutokana na changamoto hizo, DCB tulianzisha bidhaa hii maalum ya mpango wa elimu inayomuwezesha mtoto kusoma hadi kumaliza elimu ya chuo kikuu bila ya shida yoyote”, aliongeza mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo alisema akaunti hiyo inampa fursa mteja kuchagua muda wa kuweka akiba kuanzia mwaka 1 hadi 17 na endapo atapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kabla ya muda kwisha, mtegemezi hurudishiwa kiasi cha fedha alichoweka kuanzia mwanzo wa mpango na vilevile mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba.
Kuhusu maendeleo ya benki Bwana Ndalahwa alisema DCB imeweka kipaumbele katika kusaidia jamii hususani kwenye utoaji wa elimu na mitaji midogo midogo kwa wananchi wa kipato cha chini ambapo hadi mwishoni mwa Disemba 2018 imeweza kutoa mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 160 kwa wafanyabiashara wadogo wa vikundi ikiwemo shilingi bilioni 16 zilizotolewa kwa mfuko wa wanawake na vijana wa halmashauri za Jiji la Dar es Salaam kupitia njia ya ukopeshaji wa vikundi vidogo.
“Mikopo hii yenye masharti na riba nafuu imeleta chachu katika kuendeleza jamii kwani imewasaidia wazazi kufanya biashara na kusomesha watoto wao. Benki imetoa mikopo kwa zaidi ya watanzania 38,000 ambao wananufaika na huduma hizi. DCB pia ndio benki ya kwanza kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali na kupitia mikopo hii wafanyakazi hawa wameweza kuimarisha maisha yao”, alisema.
Pamoja na mikopo hiyo alisema DCB pia imeendelea kutoa mikopo ya nyumba za bei nafuu kwa watanzania ambao maeneo yao hayajapimwa na wanaamini kupitia mikopo hii pia wazazi wameweza kujenga nyumba zao na kusomesha watoto, yote hiyo ikiwa ni katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha watanzania wanaishi maisha bora.
“Benki ya DCB itaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa elimu katika mambo yenye kuleta maendeleo ya sekta za elimu nchini na tungependa kutoa pongezi zetu kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri katika mitihani ya taifa kwani washahili walisema ‘Mcheza kwao hutunzwa’ na leo tunawatunza”, alisema.
No comments