Breaking News

Benki ya DCB yazindua akaunti maalumu ya elimu iitwayo DCB Skonga

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa akaunti maalum ya akiba ya mpango wa elimu ijulikanayo kama ‘DCB Skonga’ inayolenga kumhakikishia mteja kuweka akiba na uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufika Chuo Kikuu. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Balozi wa akaunti hiyo, Zamaradi Mtetema, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko na Mkuu wa Msoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa.  

DCB YAZINDUA DCB SKONGA – FURSA MPYA YA ELIMU KWA WATANZANIA HADI CHUO KIKUU

Dar es Salaaam Oktoba 9, 2019. BENKI ya Biashara ya DCB imezindua akaunti maalumu ya akiba ya mpango wa elimu ijulikanayo DCB SKONGA ikilenga kumhakikishia mteja kuweka akiba na uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu.
Akizungumza katika uzinduzi wa akaunti hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Ndugu Godfrey Ndalahwa alisema, ‘’DCB Skonga ni akaunti maalum ya akiba inayompa mteja fursa ya kuweka akiba kila mwezi ili kutimiza malengo aliyo jiwekea huku mteja akihakikishiwa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu. Benki ya DCB tunaamini katika kutoa fursa zenye tija kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla kwa kuja na bidhaa nzuri zinazowapa tija na faida lukuki. Alisema ‘Kwa mara nyingine tena leo DCB inaandika historia nyingine kwa kuzindua bidhaa mpya ya mpango wa elimu ijulikanayo DCB SKONGA AKAUNTI’’

Mkurugenzi mtendaji wa benki hio aliongeza ‘‘kumekuwa na changamoto kubwa sana katika jamii inayotuzunguka pindi mzazi/mlezi anaetegemewa na familia anapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu, kwani watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo hii imetengeneza hofu kwenye familia nyingi’’. 

‘’Kutokana na changamoto hizi, DCB tumekuja na bidhaa hii maalum ya mpango wa elimu itakayo muwezesha mtoto/watoto kusoma hadi kumaliza elimu yao ya chuo kikuu bila ya shida yoyote’’. Akaunti hii maalum ya akiba inamuwezesha mteja kuweka akiba kidogo kidogo kila mwezi kulingana na mpango na gharama za masomo ya mtoto wake’’

Mkurugenzi mtendaji aliongeza ‘’Uzinduzi huu wa akaunti maalumu ya akiba ya DCB Skonga ni moja ya utekelezaji wa  mpango mkakati wa miaka mitano tuliojiwekea katika kukuza na kuendeleza benki ya DCB katika kutoa fursa na bidhaa zenye tija kwa wateja wetu. Elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu hivyo tunaamini watanzania watakimbilia fursa hii ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao’’.
Nae Mkurugenzi wa Biashara Ndugu James Ngaluko aliongeza ‘’kupitia bidhaa hii ya DCB Skonga  mteja anaweza kuchagua mpango wa aina mbalimbali wa kuweka akiba pamoja na muda wa uwekezaji  kulingana na umri, gharama na muda wa masomo ya mtoto wake’’.
Akizungumza zaidi kuhusu DCB Skonga, Mkurugenzi wa Biashara alisema, ‘’ Hii ni njia salama ya kuweka akiba yako huku ukihakikishiwa elimu ya mtoto wako na mwisho wa muda ulio chagua (mwaka mmoja hadi kumi na saba) benki itakupa akiba yako yote ambayo pia itakusaidia kutimiza malengo yako mengine mbalimbali ya kimaisha’’.

Alisema akaunti hii inampa fursa mteja kuchagua muda wa kuweka akiba kutoka mwaka 1 hadi 17 na endapo atapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kabla ya muda kuisha, tegemezi wako watarudishiwa kiasi cha fedha ulicho weka kuanzia mwanzo wa mpango na vilevile mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba.

“DCB Skonga ni njia nyingine ya juhudi za benki katika kusapoti juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Joseph Pombe Magufuli katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanakwenda shule na kupata elimu bora.“Lakini mbali na hilo, DCB tunaamini endapo mteja wetu hatakua na hofu ya maisha yake ya baadae pamoja na elimu ya watoto wake, basi ataongeza kiwango cha uzalishaji mali hivyo pia kuboresha uchumi wake binafsi na wa taifa”, aliongeza Mkurugenzi Mtendaji.

Akizungumza zaidi faida ya akaunti hiyo mpya, mkurugenzi wa biashara Bwana James Ngaluko alisema, akaunti hii inatoa fursa kwa kila mtanzania na kiwango cha chini kabisa cha uwekezaji kila mwezi ni shilingi elf tano (5000) vilevile mteja anakuwa na uhakika wa usalama wa pesa zake, uhakika wa elimu ya mtoto hadi chuo kikuu, gawio nono la kila mwaka, uhakika wa mkopo wa dharura hadi asilimia 50 ya kiwango cha akiba, bima ya mazishi endapo mwenye akaunti/mume/mke au mtoto atakapofariki na hakuna gharama za uendeshaji wa akaunti .

“Wazazi walindeni watoto wenu, wekeni mazingira bora ya maisha ya baadae, na njia pekee ya kuwezesha hili ni kujiunga na akaunti ya DCB Skonga kwani licha ya manufaa ya elimu kwa watoto wako, endapo ukichangia kwa kipindi chote cha mkataba bila kusitisha kwa sababu yoyote, benki itakurudishia amana zako zote ulizowekeza hivyo kukupa fursa zaidi ya kujiendeleza”, aliongeza mkurugenzi huyo.

Uzinduzi wa akaunti ya DCB Skonga ni mwendelezo wa juhudi za benki katika kuboresha maisha ya wateja na watanzania kwa ujumla katika kuhakikisha inaingiza bidhaa na huduma bora zinazoakisi maisha halisi ya watanzania, hivi karibuni benki ilizindua huduma za DCB Lamba Kwanza, DCB Sokoni zote zikiwalenga watanzania wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara wa ngazi zote. Mteja anaweza kutembelea tawi lolote la DCB ili kujiunga na akaunti ya DCB Skonga na kuanza kufuatilia mpango wake wa uwekezaji.

 Kwa maelezo zaidi wasiliana na
DCB Commercial Bank

+255 22 217 2197/info@dcb.co.tz     

No comments