WAJASILIAMALI WADOGO NCHINI WAISHUKURU TLED
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (katikati), akipata maelezo kutoka kwa mmoja mjasilia mali mdogo na wawanufaika wa mradi huo Anchila Petro (kulia), wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam. (Kushoto) ni Mjasiliamali na mnufaika wa wa TLED Sitta Tumma.
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (kulia), akionesha moja ya Bidhaa iliyoandaliwa na Mashine waliotoa msaada kwa Mnufaika na mjasiliamali Selena Chibando wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaamwengine ni wajasilia mali na wanufaika wa TLED.
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (katikati), akiuliza jambo kwa Mjasiliamali mdogo na mnufaika wa mradi huo Mariamu Juma, (kushoto) wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam kulia ni mjasilia mali na mnufaika wa TLED.
The Tanzania Local Enterprise Development (TLED) ni mradi wa ni uliandaliwa kwa miaka mitano (April 2015 – Machi 2020) unaofadhiliwa na Global Affairs Canada (GAC).
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Bi Jemima Michael, anasema TLED ni mradi maalumu kwa Wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo na wakati, katika kukabiliana na vikwazo vya biashara vinavyowakabili hasa upatikanaji na ukuaji wa masoko katika sekta ya biashara ya kilimo, kwa kuzingatia changamoto za ziada zinazowakabili wanawake wajasiriamali.
Bi Jemima ameongeza kuwa TLED nia yake kuu ni kutoa rasilimali muhimu za biashara kwa wajasiriamali wa ndani ili kuongeza ajira endelevu kwa wanawake na wanaume katika sekta ya biashara ndogo na ya kati, na kuboresha utoaji wa ajira kutokana na maendeleo na huduma za kifedha kwa wajasiriamali katika mikoa sita nchini.
Mikoa iliyofaidika na mradi wa TLED ni Shinyanga, Mwanza, Lindi, Mtwara, Iringa na Njombe huku malengo mahususi ni kuhakikisha mnufaikaji wa mradi huo anapatiwa elimu na ushauri kutoka kwa timu ya washauri wakuu (wanaojitolea) na wafanyakazi wa mradi.
Aidha Bi Jemima aliongeza kuwa TLED huakikisha wanufaikaji wa mradi huu wanaunganishwa na soko la biashara zao, upatikanaji wa teknolojia na upatikanaji wa fedha kwaajili ya kuendeshea biashara hizo.
Awali Afisa huyo alielezea malengo ya mradi huo ni kuwafikia wajasiriamali 1760 mpaka ukomo wa mradi huo, ambapo kwasasa mradi huo umeweza kuwafikia watu 1361 sawa na 77% ya walengwa wote wa mradi.
Kupitia maonesho haya ya Sabasaba tumeyatumia kuwapa fursa wajasiliamali kujifunza kwa kuona wenzao wanafanya nini na kuzitangaza biashara zao kimataifa kupitia jukwaa hili la maonesho ya sabasaba, aliongeza Bi Jemima Michael.
Bi Careen Charles, mjasiriamali wa kutengeneza mikoba asili kutokea shinyanga ameushukuru mradi wa TLED kwa kumpa fursa ya kushiriki katika maonesho ya sabasaba, na kumsaidia kupata soko la biashara zake la uhakika.
No comments