Breaking News

Sanlam yakabidhi madarasa na ofisi za walimu Kondoa

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakishikana mikono baada ya kufungua pazia la jiwe la msingi katika uzinduzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu  ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma (wa pili kulia) na Meneja wa Mamlaka hiyo kanda ya kati, Stella Rutaguza (kulia).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu  ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA),  DK.  Mussa Juma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakifungua pazia la  jiwe la msingi kuzindua   madarasa mawili na ofisi ya walimu  ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam yenye thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka Kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Stella Rutaguza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili  na Ofisi ya walimu  ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Makabidhiano yalifanyika shuleni hapo,  Pahi, Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akihutubia katika hafla ya uzinduzi pamoja na makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu  ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa  Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman akihutubia katika hafla ya uzinduzi pamoja na makabidhiano ya madarasa mawili  na ofisi ya walimu  ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati waliokaa ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji na kushoto kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma.

Watanzania hawana budi kuchukulia bima kama hitaji muhimu na kujifunza aina mbalimbali za bidhaa za bima zilizopo sokoni ili wazitumie kujikinga, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatu Kijaji amesema hivi karibuni akiwa ziarani wilayani Kondoa, Mkoani Dodoma.

Waziri huyo alitoa wito huo wakati wa hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya madarasa mawili, ofisi ya walimu na madawati 40 vyenye thamani ya jumla ya Tsh 49m kwa shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani Kondoa, vilivyojengwa kwa msaada wa kampuni ya bima ya Sanlum, ambayo ndiyo mtoaji mkubwa wa bima barani Afrika.

 “ Huduma ya bima inahitajika sana ili kuwawezesha watu kujikinga na majanga yasiyotabirika ya siku za usoni,” alisema Dr. Kijaji, na kuongeza kuwa ishara iliyoonyeshwa na kampuni ya Sanlam ya kurudisha sehemu ya faida  yake kusaidia miradi ya jamii ichukuliwe kama ishara ya namna gani bima ni muhimu kwa uhakika wa maisha.

Akiongea katika hafla  hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda – Afrika Mashariki wa Sanlam Pan-Afrika, Julius Magabe, alisema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi ya jamii nchini Tanzania.

 “ Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia kuwa Sanlam tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutoa fedha kwa miradi mbalimbali ya jamii”, alisema Magabe, nakuongeza kuwa kampuni hiyo – ambayo imesherehekea mwaka 2018 imesherehekea miaka 100 tangu kuanziswha kwake, iko thabiti katika kurejesha sehemu ya faida yake kusaidia jamii.

Awali akiongea katika hafla hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lusangi, Josephine Paul, alisema shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa, kwa kuwa madarasa matano yaliyokuwepo kabla hayakuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi ambayo ni 348.

“Kutokana na mradi huu kukamilika, utakuwa umepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa na oofoso ya walimu uliokuwepo,” alisema mkuu huyo wa shule.

Na katika hali ya kuonyesha ufanisi nadra katika matumizi ya fedha za wafadhili kitendo ambacho kilimvutia waziri Dr. Kijaji na vilevile ujumbe wa Sanlam, ujenzi huo siyo tu ulikamilika ndani ya muda uliopangwa, bali zaidi ya Tsh 2.7m zimeokolewwa kutokana na kupunguza gharama, fedha ambazo zimewekezwa katika ujenzi wa vyoo wa wanafunzi wa kike na wa kiume.

 “ Sisi Sanlam hatujawahi kushuhudia mradi tunaoufadhili ukisimamiwa kwa umakini wa hali ya juu kiasi hiki,” Alisema Magabe, ambayo kampuni anayotumikia ina matawi ndani ya nchi 38 barani Africa, huku huduma zake zikiwa zimesambaa mabara ya Amerika, Asia na Australia


No comments