Breaking News

Uzinduzi wa reli ya Tanga- Moshi utaongeza kipato kwa mikoa ya kaskazini


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kulia), akimsikiliza Meneja Kiwanda cha Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kushoto) katika hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor na Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo.
Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa (kulia) wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor, Meneja Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema na Meneja Mauzo Taifa wa kampuni hiyo, Leslie Massawe.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa (kulia) akishikana mikono na Meneja Mauzo Taifa wa kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Leslie Massawe wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor, Meneja Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Tanga Cement, Diana Malambugi na Meneja Biashara wa Kampuni hiyo, Peet Brits.

Meneja Kiwanda cha Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akipunga mkono kwa baadhi ya wakazi na mashuhuda wengine waliofika katika uzinduzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wakazi wa Moshi na wananchi wengine wakiangalia treni la kwanza la mizigo lililobeba saruji ya Tanga Cement baada ya kuwasili katika  stesheni ya Moshi wakati wa uzinduzi wa safari za treni hiyo litakalofanya safari zake katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga (TCPLC) pamoja na washuhudiaji wengine wakihudhuria uzinduzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar - Tanga - Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Uzinduzi wa reli ya Tanga - Moshi utaongeza kipato kwa mikoa ya kaskazini

Na Mwandishi wetu, Moshi

Uzinduzi wa huduma za reli kati ya Tanga na Moshi utaongeza kipato kwa mikoa miwili hiyo, kuchagiza kukua kwa sekta  ya ujenzi majumba  na zaidi kuifanya Tanga ijitwalie hadhi yake ya zamani enzi za  kilele cha zao la katani katika soko la dunia, ambapo Tanga ulikuwa  ni mji maarufu, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement  Reinhardt Swart akiongea kuhusu uzuduzi huo.

Kampuni ya Tanga Cement ilikuwa ni mteja wa kwanza wa huduma hizo mpya ambazo zilisita miaka 12 iliyopita, ambapo treni hiyo iliwasili katika stesheni ya treni ya moshi mjini ikikokota mabehewa yaliyosheheni jumla ya tani 800 kwa mpigo, mzigo ambao ni swan a ule ambao ungesafirishwa na malori 30.

“Ninaamini usafirishaji kwa urahisi wa  bidhaa kati ya vituo hivyo viwili utaongeza kiwango cha watu kuzalisha kipato kwa mikoa yote miwili. Sisi tunahitaji watu wengi zaidi wajipatie pesa mifukoniu mwao ambayo itawasaidia kujenga nyumba bors ambazo bila shaka zinahitaji aruji, hivyo tutaongeza mauzo yetu, kuonheza kipato cha wanahisa wetu kupitia gawio, serikali ya Tanzania itavuna kodi ambayo itasaidia  katika maendeleo ya nchi,” alisema mkurugenzi huo.

Aliongeza kuwa Tanga ni eneo muhimu la kiuchumi  na ina miundombinu yote muhimu ambayo ni bandari, barabara na reli. Wahusika wakivisimamia hii miundombinu vyema na kuitumia ipasavyo, alisema ana uhakika kuwa ‘ baada  ya mika michache, tanga itakuwa zaidi ya ilivyokuwa enzi zake za kilele cha katani, kitu kilichofanya Tanga uwe ni mji maarufu  nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Kampuni ya Tanga Cement ni kati ya wateja wakubwa wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRC) na mwaka 2016 illisaini mkataba wa iliyokuwa TRL kuwezesha usafirishaji wa saruji kutoka Tanga Cement kuwaendea wateja wa kampuni hiyo waliopo mikoa ya Mwanza na Kigoma.  

Mkataba huo wa makubaliano ulitiwa saini ili kuwezesha usafirishaji wa zaidi ya tani 35,000 za saruji kwa mwezi. Kampuni ya Tanga cement ilitengewa vichwa vitano vya treni na kichwa cha treni cha kupangia mabehewa ili kuwezesha usafirishaji watani 20,000 kwa mwezi kutoka Ponge hadi kigoma, na tani 15,000 kwenda mwanza.

“Hii ilikuwa ni hatua muhimu ya mafanikio katika kupatia ufumbuzi usafirishaji wa saruji. Tumejenga uhusiano mzuri sana na TRC ambapo tunakutana mara kwa mara  kuhakikisha kuwa kila jambo linakwenda sawia hasa kuhusiana na utekelezaji wa mkataba huo  wa makubaliano na tunatoa mapendekezo yanapohitajika na kushauri marekebisho ya hapa na pale, aliongeza Ndugu Swart.

Kukua kwa ujenzi wa mjumba mbao mkurugezi huyo wa Tanga cement  anautabiri siyo ndoto ya alinacha, kwa kuwa wadau wanakubaliana kuwa  matumizi ya reli katika kusafirisha saruji kutapunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa ujenzi, na hivyo kusababisha bei ya saruji kushuka.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa wachambuzi wa kimataifa wanakadiria kuwa kutumia reli badala ya barabara kunapunguza gharama za usafirishaji kwa  kiwango cha asilimia 30-40.

Kwa mujibu wa wadau wa sekta ya usafirishaji, kusafirisha tani moja ya saruji kutoka Tanga hadi Moshi kwa barabara kunagharimu Tsh 40,000, wakati reli inakadiriwa kugharimu Tsh 28,000. Tanga Cement yenyewe inatarajia kusafirisha jumla ya tani 1,600 kwa wiki na 80,000 kwa mwaka kutoka kiwandani Tanga hadi Moshi.

Waziri Mkuu Majaliwa Alisema “Usafiri wa reli ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi nchini, kwa kutumia reli, inawezekana kusafirisha  bidhaa nyingi kwa wakati moja. Nina hamu ya kuona kuwa watu wanatumia fursa hii ya huduma ya reli kuagiza bidhaa, na bila shaka bei ya bidhaa itapungua”

Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mwenyekiti wa Bodi wa TRC Prof. Kondoro, naye alichangia swala la reli kupunguza gharama, na akasema kuwa kuziduliwa kwa huduma za reli kati ya Tanga na Moshi ni sehemu ya mkakati wa serikali na TRC kuhakikisha kuwa gharama za usafirishaji wa bidhaa zinapungua, kama njia ya kusaidia kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Alisema Prof. Kondoro “Uzinduzi huu ni  sehemu ya mkakati madhubuti wa kuona kwamba tunasafirisha bidhaa kwa gharama nafuu, na kwa kuwa kutumia reli kunapunguza gharama za usafirishaji, hii itasababisha bei za bidhaa kushuka sokoni.  

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa TRC Masanja Kadoigosa, kwa mara ya mwisho treni ya mizigo kwenda Moshi kutokea Tanga, umbai wa km 438, ilikuwa mwaka 1993, huku treni ya abiria ikisitisha safari zake  mwaka 1994.

Ujenzi upya wa reli  ya  Tanga – Moshi ulianza mwaka 2017 na kukamilika mwaka 2019, na ulijumuisha wafanyakazi 525, wahandisi 12, vibarua 466 na wafanyakazi maalum 47, huku mitambo zaidi ya 43 ya aina mbalimbali ikitumika, alisema Kadogosa.




Mtandao wa reli Tanzania umetambaa juu ya jumla ya maili 2707, ukipita juu ya madaraja  zaidi ya 3,000 na vituo 126, alisema mkurugenzi huyo wa TRC ndugu Kadogosa.

No comments