NBC yadhamini Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyaya (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Maonyesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akisaini kwenze kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Maonesho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Majimaji mjini Songea MKoani Ruvuma mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto kwa waziri ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, Ofisa Mauzo, Jennifer Peter, pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC, Hilaria Mhagama.
03: Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Hilaria Mhagama alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea Simon Ntwale, na Ofisa Mauzo wa benki hiyo, Jennifer PeterNaibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Jennifer Peter alipotembelea banda la NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC Songea, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema Maonesho ya Viwanda na kongamano la uwekezaji Ruvuma litaleta fursa nyingi za kibiashara na uchumi mkoani humo imeelezwa mjini Songea mwishoni mwa wiki.
Alisema Mkoa wa Ruvuma umejaliwa kuwa na fursa nyingi sana na kwa muda mrefu hawakuwa wakifanya tukio kama hilo lakini sasa kupitia kongamano hilo litawafungua kuwafahamisha watu mbalimbali kuwa nini kinapatikana mkoa huo wa Ruvuma.
Alisema changamoto zinazowakabili wawekezaji wadogo ni pamoja na upatikanaji wa mitaji lakini kwa sasa mkoa wa Ruvuma umepata mkombozi hususani Benki ya NBC ambayo inatoa mikopo mikubwa na midogo kwa masharti nafuu sana kinachotakiwa ni uaminifu.
"Nawakaribisha sana wawekezaji na wadau wote ambao wana nia thabiti ya kuja kuwekeza Ruvuma kwani mkoa huu umekuwa na nishati ya umeme ya kuridhisha inayoweza kukidhi mahitaji," alisema.
Kwa upande wake Meneja wa Tawi la NBC Songea,Simon Ntwale amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa fursa nzuri kwa Benki ya NBC kwa sababu wameweza kukutana na wadau mbalimbali watakaoweza kufungua fursa mbalimbali za kibiashara.aziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa huo amesema kuwa Ruvuma itakuwa na wawekezaji mbalimbali .
Alisema NBC imepata faida ya kuingia mkataba na taasisi ya PASS ambapo wanakwenda kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya kilimo ambapo mkopaji anaweza kupata pembejeo za kilimo.
Ntwale pia amewatoa shaka wakulima wakubwa na wadogo pamoja na wachakataji na wawekezaji wadogo kujitokeza kwa wingi ili kupata mkopo endapo kampuni ya PASS itakuwa imeadhinisha kwa mteja husika kupata mkopo huo.
"Wawekezaji na wakulima wadogo msiogope kuitumia Benki ya NBC kwani ni benki yenu ambayo ipo tayari kuwasaidia ili mtimize malengo yenu kwani wengi wamenufaika na mikopo hiyo hadi sasa wanafanya biashaza za mazao yao hadi nje ya nchi," alisema.
No comments