WATAALAM WAWASILISHA USANIFU WA AWALI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA MSALATO DODOMA
Meneja
Mipango na Usanifu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mohamed Millanga
(wa kwanza kushoto), akiangalia moja ya picha (hazionekani pichani) za usanifu
wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo
na Wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa Kampuni ya Studi ya Tunisia
kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA),
ambapo uliudhuriwa na wataalam mbalimbali wa usafiri wa anga.
Wahandisi
Kamel Fazhani (kulia) na Marrarchi Walis (kushoto) wa Kampuni ya Studi ya
Tunisia wakiwasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Msalato Dodoma leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA), mbele ya wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa
anga.
Mhandisi
Bernard Kavishe (aliyesimama) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),
akichangia hoja katika mkutano uliofanyika leo wa uwasilishaji wa usanifu wa
awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), ambapo umewasilishwa na wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
Mwonekano
wa Jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma,
uliowasilishwa leo katika usanifu wa awali kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na wataalamu kutoka Kampuni
ya Studi ya Tunisia.
Said
Mpwili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) (nyuma aliyenyanyua
mkono), akiwasilisha mapendekezo ya ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege kwa
wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia, ambao leo katika ukumbi wa
mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
wamewasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato
Dodoma.
No comments