WAJASIARIAMALI WA KIVULE NEEMA YAWASHUKIA
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) kata ya Kivule,Bihimba Mpaya (wapili kulia) akizungumza
na wafanyabiashara wadogo wadogo wa kata hiyo (hawapo pichani) jijini Dar es
Salaam leo katika kikao cha tatu cha kuongea na wajasiriamali hao juu ya
kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba kutoka kwa Meya wa jiji Mhe.Isaya Mwita.Mikopo
hiyo itatolewa kwa vikundi vya watu wanne wanne ambao watapewa shilingi Milioni
tatu (3,000,000) watagawana kila mmoja Shilingi laki Saba na Hamsini (750,000)
ambapo kila mtu mmoja atarudisha kwa mwezi shilingi 62,500 kwa watu wanne itakuwa ni Shilingi 250,000/= kwa
mwaka itarudi pesa ile ile bila riba.Meya wa jiji ametoa hizi pesa kutoka
katika miradi ya jiji kwa dhumuni la kuinua wafanyabiashara wadogo wadogo kwani
wafanyabiashra wengi wanashindwa kuendeleza biashara zao kutokana na kukopa
kwenye mabenki kwa riba kubwa hivyo basi wanaposhindwa kulipa hufilisiwa
biashara zao na vitu vingine.
Diwani wa Kata ya Kivule kupitia Chama cha
Deomkrasia na Maendeleo (Chadema), Wilson Molel (wapili kulia) akizungumza na
wafanyabiashara wadogo wadogo wa kata hiyo katika kikao cha tatu cha kujadili
suala la kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba kutoka kwa Meya wa Jiji, Mhe.Isaya
Mwita kwa Vikundi vya watu wanne wanne ambvyo wanachama wavikundi hivyo
watakopeshwa Shilingi Million tatu.Kutokana na vikundi hivyo kukosa ujuzi
pamoja akaunti za vikundi Katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Kivule,Ndugu
Bihimba aliwaalika maofisa kutoka katika Benki ya Yetu Microfinance Bank Plc
kwa ajili ya kutoa semina ya kuendesha biashara katika vikundi pamoja na
kuwafungulia akaunti za Vikundi ambapo zoezi hilo litaanza Jumatatu Tarehe 28
katika kata ya Kivule.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya Yetu
Microfinance Bank Plc wakitoa semina kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa kata
ya Kivule jijini Dar es Salaam leo juu ya kufungua akaunti za vikundi pamoja na
mikakati kuendesha biashara zao.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo
wadogo wa kata ya Kivule wakisiliza kwa makini mada zitolewazo na Diwani wa kata
ya Kivule, Wilson Molel, Katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Kivule, Bihimba
Mpaya na Maofisa walioalikwa na Katibu kutoka katika Benki ya Yetu Microfinance
Bank Plc katika kikao hicho.Huo ni mwendelezo wa viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo kupambana katika kuinua uchumi pamoja na kupunguza
idadi ya vijana wanaokosa ajira katika kata ya Kivule.
No comments