WAITARA APAMBANA NA KERO YA BEACH PEMBA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (alievaa shati la madoa madoa) akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na wakazi wa kata ya Mzinga katika ukaguzi wa moja ya chemba ya mradi wa kutoa maji ya mvua yanayotuama iliyochimbwa maeneo ya Kitunda Nyangasa jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kushoto)
akizungumza na wakazi wa Beach Pemba kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam jana
baada ya kuwasili katika kata hiyo katika hafla ya ukaguzi wa mradi wa kutoa
maji ya mvua yanayotuama katika eneo hilo pamoja na kusikiliza kero kutoka kwa
wakazi wa kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita
Waitara (watatu kushoto) akiongozana na viongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kata ya Mzinga baada
ya kuwasili katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya ukaguzi wa
mradi wa ujenzi wa mifereji ya chini kwa chini inayotoa maji kutoka katika makazi
ya watu Beach Pemba na kumwaga Bonde la Mto Mzinga.
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kata ya Mzinga
wakimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga,
Mwita Waitara (katikati) moja ya chemba ya mifereji ya chini kwa chini inayotoa
maji kutoka Beach Pemba na kumwaga katika Bonde la Mto Mzinga.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kushoto)
akisalimiana na wahanga wa Beach Pemba kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam jana
baada ya kuwasili katika kata hiyo kwa ajili ya Ukaguzi wa mradi wa mifereji ya
chini kwa chini inayotoa maji ya mvua
yanayotuama katika eneo hilo na kumwaga katika Bonde la mzinga.Ni mwendelezo wa
Mbunge kutimiza ahadi alizoahidi kwa wakazi wa kata ya Mzinga.
Diwani wa kata ya Mzinga,Job Isaack (aliyevaa
shati la bluu) akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara Maji
yaliyotuama katika eneo la makazi ya watu Beach Pemba.
No comments