BONANZA LA WAITARA LAPAMBA MOTO MSONGOLA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akipiga
penati kuashiria ufunguzi wa Bonanza la Mpira wa miguu liliodhaminiwa na Mbunge
huyo lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mvuti jijini Dar es Salaam
jana.Bonanza hilo limehusisha timu 12 kutoka katika mitaa ya kata ya Msongola
ambapo washindi wawili kati ya timu hizo watapata nafasi ya kuingia katika ligi
ya Jimbo la Ukonga ambayo itahusisha washindi wote kutoka katika kata 13 za
jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara
(kushoto) akizungumza na wachezaji wa timu za mpira wa miguu jijini Dar es
Salaam jana katika Bonanza la Mbunge huyo lilifanyika katika uwanja wa Shule ya
Msingi Mvuti iliyopo katika kata ya Msongola.
Mbunge a Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara
(kustoto) akipeana mikono na wachezaji wa Timu ya Toto Fc Kitonga katika
Bonanza hilo.
Mchezaji wa Timu ya Toto Fc Kitonga, Michael
Samuel (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Mvuti Fc, Frank Daniel
katika mchezo wa fainali ya Bonanza la Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara
lililofanyika katika uwanja wa Shule ya msingi Mvuti jijini Dar es Salaam jana.Ni
mwendelezo wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga kutekeleza ahadi alizoahidi kwa vijana
juu ya kuinua sekta ya michezo kwa wakazi wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia)
akikabidhi jezi na mpira kwa Kapteni wa Timu ya Toto Fc Kitonga, Rajabu
Saidi baada ya kuibuka mshindi kwa kuipiga bao 1-0 timu ya Mvuti Fc katika
fainali ya Bonanza la Mbunge huyo lililofanyika katika uwanja wa Shule ya
msingi Mvuti kata ya Msongola jijini Dar
es Salaam jana.Katikati ni Msimamizi wa Bonanza hilo na pia ni Katibu Msaidizi wa chama cha mpira wa
miguu Wilaya ya Ilala (IDFA), Hugo Seseme.Huu ni mwendelezo wa Mbunge wa jimbo la Ukonga kutimiza ahadi
alizoahidi kwa wakazi wa jimbo hilo juu ya kuinua sekta ya michezo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia)
akikabidhi jezi pamoja na mpira kwa Kapteni wa Timu ya Mvuti Fc, Emmanuel
Steven baada ya kuibuka mshindi wa pili katika Bonanza la Mbunge huyo
lililofanyika katika uwanja wa Shule ya msingi Mvuti kata ya Msongola jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni
Msimamizi wa Bonanza hilo na pia ni
Katibu Msaidizi wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Ilala (IDFA), Hugo Seseme.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia)
akikabidhi mipira miwili kwa Kapteni wa Timu ya Sokoine Fc, Amiri Omary baada
ya kuibuka mshindi wa tatu katika Bonanza la Mbunge huyo lililofanyika katika
uwanja wa Shule ya msingi Mvuti kata ya Msongola jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni
Msimamizi wa Bonanza hilo na pia ni
Katibu Msaidizi wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Ilala (IDFA), Hugo Seseme.
No comments