WANAWAKE WATUMIA MASHIRIKA KUPIGANIA 50 KWA 50 KWA KATIKA NAFASI ZA UAMUZI
MASHIRIKA mbalimbali
nchini yametumia maadhimisho ya Siku ya Wanawake kuungana kujadili nafsi ya
mwanamke kwa lengo la kuleta matokeo chanya hasa yanayohusu usawa wa asilimia
50 kwa 50 katika nafsi za uamuzi huku wakijadili kwa kina namna ya kuondoa
changamoto zinazowakabili wanawake.
Baadhi ya mashirika hayo
ni Shirika la Umoja wa Ulaya (EU), Save the Children, Plan International
Organization, Femina Hip, Allience Francaise na Usawa Tanzania ambapo leo
wamekutaja jijini Dar es Salaam kujadili mambo yanayohusu wanawake ikiwa ni moja
ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Machi 8
ya kila mwaka.
Akizungumza wakati
maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Balozi wa Ufaransa nchini amesema Tanzania
imepiga hatua katika kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na amehaidi kuwa
bega kwa bega kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa mtoto wa kike.
Kwa upande wake
Mwanasaikolojia na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Chris Mauki,
amefafanua kukutana kwa mashirika hayo pamoja na mambo mengi wamelenga
kuwapongeza wanawake wote walio katika sekta mbalimbali hasa katika kuleta
maendeleo katika jamii.
Wakati maadhimisho,
mashirika hayo yamejadilia mambo kadhaa likiwamo la kuangalia nafasi ya
mwanamke katika kupewa kipaumbele ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey
Polepole amesema suala la kuwaweka wanawake mbele halina mjadala.
Amefafanua ni kwasababu
wanawake wamekuwa bora kuliko wanaume hasa kwenye masuala ya kufikiri na
kutekeleza majukumu yao kwenye jamii na kutumia maadhimisho hayo kuwatakia
mafanikio mema wanawake wote katika kutelekeza majukumu yao huku akielezea huu
si wakati wa kuendelea kufanya unyanyasaji kwa wanawake.
“Kutoa kipaumbele kwa
wanawake halihitaji mjadala kwani wamekuwa bora katika maeneo yao ya kazi
kuliko ambavyo wamekuwa wanaume walio wengi.Wamekuwa ni watu wakufikiria katika
mtazamo chanya wanapotekeleza majukumu yao,"amesema Polepole.
Amependekeza mbinu za
kumkomboa mtoto wa kike na baadhi ya mbinu hizo ni kumpatia elimu mtoto
wa kike ambayo itamkomboa na kutoruhusu mtu yeyote kutocheza na mtoto wa shule
kwa namna yoyote.
Wakati huohuo, Mkurugenzi
wa Children Dignity Forum (CDF), Koshuma Mtengeti amesema ukatili kwa mtoto wa
kike kwa sehemu kubwa umekuwa ukifanyika majumbani na kuomba watumie nafasi
hiyo kujikita kuangalia namna bora za kuondoa changamoto zinazomkabili mtoto wa
kike nchini.
No comments