WAITARA AWAPA MOTISHA VIJANA KATIKA MICHEZO
Mbunge
wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akizungumza na wakazi wa mtaa wa Rubakaya
iliyopo kata ya Zingiziwa katika fainali ya Bonanza la Baraza la Vijana wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) lenye lengo la kuhamsisha juu ya
zoezi la kufanya usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko
lililofanyika katika Viwanja vya Kimyakimya jijini Dar es Salaam jana.
Mchezaji
wa Timu ya Sisi ndio Sisi Fc,Shiyo Msenga (kulia) akijaribu kumtoka mchezaji wa
timu ya Shado Fc,Ibrahimu Mkwege katika fainali ya Bonanza la Baraza la Vijana
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) lenye lengo la kuhamsisha zoezi
la kufanya usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko
lililofanyika katika Viwanja vya Kimyakimya jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Baraza
la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha),Rodgers Nyagani akitoa shukrani za
dhati kwa Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita
Waitara baada ya kuwasili katika Bonanza hilo ili kukabidhi zawadi ya
mipira miwili kwa Mshindi wa kwanza na mpira mmoja mmoja kwa timu nane (8) zote
zilizoshiriki katika michuano hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Kimyakimya
jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Shado Fc na Sisi ndio sisi Fc wakimsikiliza kwa makini
Mbunge wa jimbo la Ukonga.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (wapili kushoto) akimkabidhi zawadi ya mpira
kwa washindi wa pili,Timu ya Sisi ndio Sisi Fc katika Mashindan ya Bonanza la
Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) yenye
lengo la kuhamasisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira ili kujikinga na
magonjwa ya mlipuko lililofanyika katika Viwanja vya Kimyakimya jijini Dar es
Salaam jana.Katikati ni Mwenezi wa kata ya Kitunda,Nelson Muro.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (kushoto) akimkabidhi zawadi ya mipira miwili
kwa washindi wa kwanza,Timu ya Shado Fc katika Mashindano ya Bonanza la Baraza
la Vijana wa Chadema (Bavicha) yenye
lengo la kuhamasisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira ili kujikinga na
magonjwa ya mlipuko lililofanyika katika Viwanja vya Kimyakimya jijini Dar es
Salaam jana.Wapili kushoto ni ni Mwenezi wa kata ya Kitunda,Nelson Muro.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa
timu zote mbili zilizoingia fainali,Viongozi wa Chama cah Demokrasia na
Maendeleo kutoka katika kata mbalimbali za jimbo la Ukonga na Wakazi wa mtaa wa
Rubakaya baada ya kukabidhi zawadi ya mipira kwa washindi hao.
No comments